Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Juma Sweda ameteketeza Dhana za Uvuvi haramu zenye thamani ya shillingi 127,245,000/=zilizokamatwa zikiwa zinatumika katika Shughuli za Uvuvi wa Samaki katka Ziwa Victoria kwa kipindi cha mwezi Machi 2017.
Dhana hizo za uvuvi haramu zimeteketezwa hivi karibuni Wilayani hapa,baada ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kufanya Operationi maalum ya kukamata na kuwataka Wavuvi kusalimisha kwa hiari dhana haramu kwa lengo la kutokomeza uvuvi haramu Wilayani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,amewataka Viongozi,Wataalamu na Watendaji wote wa ngazi ya Tarafa, Kata na Vijiji waliopo katika maeneo ya kandokando ya Ziwa Viictoria kuhakikisha Wanatokomeza na kuondoa Uvuvi haramu katika maeneo yao ya Kiutawala kwa kusimamia kikamilifu sheria za uvuvi na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya dhana bora na sahihi za uvuvi na utunzaji wa mazingira ya Ziwa ili kulinda Raslimali ya Uvuvi kwa lengo la kuongeza uchumi na kipato kwa Wananchi.
Amewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji husika kuhakikisha dhana haramu hazipatikani katika maeneo yao ya Kiutawala sambamba na na kudhibiti Samaki wachanga wanaovuliwa na kuuzwa katika Masoko na mialo kwenye maeneo yao.
Sweda, ameitaka Idara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha wahusika watakaopatikana na dhana haramu pamoja na Samaki wachanga wachukuliwe hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.