Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amefika kata ya mwaniko kuhamasisha Ujenzi wa Zahanati Mpya Kufuatia Kuhalibiwa na Mvua Zahanati Iliyokuwepo na Mvua Za Masika Wakati akiwapa pole Wananchi wa Kata ya Mwaniko kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo na kusababisha Majengo kubomoka ikiwemo Zahanati iliyokua ikitoa Huduma ya Afya.

Akizungumza Tarehe 15 Novemba 2025 Mhe. Samizi amesema kuwa Serikali imefika na kutazama tukio kwa ujumla na kusema suluhu la muda mfupi ni kuwa huduma za afya zitafanyika katika ofisi ya mtendaji wa kata huku jitihada za kuanza ujenzi wa zahanati ukiendelea ikiwa ni suluhu ya muda mrefu ambapo wataalamu kutoka Halmashauri watahakikisha wanafanya tathimini ili kuweza kuanza ujenzi huo mara moja.

Aidha amewataka Wananchi kuendelea kupanda miti ili iwe sehemu ya kuzuia upepo lakini pia kulinda na kutunza mazingira kwa maendeleo ya badae


Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Dkt Clement Morabu amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo na ameshukuru kwa Hatua za haraka zilizofanyika iki kuhakikisha wanaendelea na huduma ya afya.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwaniko Bw. Hezron Lutonja ameishukuru Serikali ya Wilaya kwa kufika na kuchukua hatua za uanzishwaji wa ujenzi mpya ambapo Wadau Wamejitokeza na kuchangia Mifuko 65 ya Saruji huku wakiendelea na uhamasishaji ili kuanza ujenzi huo.

Kwa upande Wake Mtendaji wa Kata ya Mwaniko Bw. Abulhaman Abeid ameshukuru hatua Mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali Ili wananchi wa kata ya Mwaniko Kuendelea kupata huduma za Afya kama kawaida .

Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.