IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI.
Halmashauri ya Misungwi ni moja kati ya Halmashauri nane (8) zilizoko katika Mkoa wa Mwanza,nyingine ni Ilemela municipality,Nyamagana municipality, Magu DC, Kwimba DC,Ukerewe DC,Buchosa DC na Sengerema DC.
Wilaya ina ukubwa wa eneo la km22,553, kati ya hizo km22,378 ni eneo la nchi kavu na km2 175 ni eneo la maji ya ziwa Victoria
Kwa mujibu ya sensa ya mwaka 2012 idadi ya watu ni 351,607 na 80% kati ya hao wanajishughulisha na kilimo na Ufugaji, 5% Uvuvi na iliyobaki ni shughuli nyinginezo. Wilaya iko nusu jangwa (semi arid) na ina mvua za vuli na masika(Bimodal rainfalls)kiasi cha 700mm hadi 1000mm kwa mwaka
Kilimo na Ufugaji ni shughuli kuu ya kiuchumi na karibu kila kaya wanamiliki mifugo
Idadi ya Mifugo Baada ya zoezi la utambuzi na usajili wa mifugo ni kama ifuaatavyo;
Miundo mbinu ya mifugo/Uvuvi ni kama ifuatavyo;
AINA |
ILIYOPO |
INAYOFANYA KAZI |
ISIYOFANYA KAZI |
Majosho
|
45 |
32 |
13 |
Minada
|
3 |
3 |
0 |
Vituo vya mifugo (Night camps)
|
1 |
1 |
1 |
Machinjio (Slaughter House)
|
1 |
1 |
0 |
Machinjio ndogo (Slaughter Slabs)
|
3 |
3 |
0 |
Makaro ya kuchinjia
|
6 |
6 |
0 |
Mabanda ya kukaushia ngozi
|
5 |
5 |
0 |
Vibanio (Cattle crushes)
|
22 |
20 |
2 |
Malambo
|
12 |
12 |
0 |
Kliniki za Mifugo –LDCs
|
6 |
6 |
6 |
Visima virefu
|
17 |
17 |
0 |
Visima vifupi
|
5 |
5 |
0 |
Mabirika ya maji (Water Troughs)
|
3 |
3 |
0 |
Mashamba ya Mifugo (Ng’ombe,Mbuzi)
|
1 |
1 |
0 |
Mashamba ya Mifugo (kuku)
|
3 |
3 |
0 |
Vituo vya uhamishaji (AI Centres)
|
2 |
2 |
0 |
Viwanda vya kuchakata Mazao ya Mifugo(Nyama)
|
1 |
1 |
0 |
Vibanio (Cattle crushes)
|
22 |
20 |
2 |
Mabwawa ya samaki (Fish Ponds)
|
123 |
110 |
13 |
Mialo (Fishing Landing Sites)
|
19 |
10 |
9 |
Vituo vya kuzalisha Vifaranga
|
3 |
2 |
1 |
Vituo vya kuzalisha mbawa kavu
|
5 |
4 |
1 |
BMU
|
10 |
10 |
10 |
Utangulizi
Idara ya Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa Idara muhimu za Halmashauri ya Misungwi. Idara hii inafanya kazi zake kwa kuakisi Dira na dhima ya Halmashauri yaMisungwi ambayo nia yake kuu ni kuinua maisha ya wananchi kwa kutoa huduma bora na kuinua uchumi wa wananchi katika Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Idara hii imeundwa na vitengo vinane ambavyo ni:
• Meat hygiene and inspection
• Hides and skin
• DSMS Animal health and Disease control
• DSMS livestock marketing Identification, Regisration and Traceability
• Fishery production • DSMS Dairy husbandry and Animal production
• DSMS Livestock extension
Kazi za Idara ya Mifugo na Uvuvi
Miongoni mwa kazi za Idara ya Mifugo na Uvuvi ni kama ifuatavyo;
1. Kufanya ukaguzi wa nyama katika machinjio na makaro ya kuchinjia ili kudhibiti magonjwa ya mifugo kwenda kwa binadamu (zoonosis )na kudhibiti nyama zisizo na ubora.
2. Kuwajengea uwezo wafugaji juu ya ufugaji bora,
3. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Samaki kwenye kata husika,
4. Kusimamia kanuni za ufugaji bora ili kuhakikisha kuwa wafugaji wanazalisha kwa tija ukilinganisha na mifugo na maeneo waliyonayo.
5. Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Mifugo na Uvuvi (K,V Mialo.Machinjio,Leseni ya vyombo vya uvuvi na wavuvi,minada nk).
6. Kuboresha Mifugo,Samaki na mazao yake kwenye maeneo husika,
7. Kutoa elimu ya ugani kwa wafugaji wa Mifugo na samaki,
8. Kutoa huduma ya chanjo za Mifugo na matibabu,
9. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Uvuvi kwenye Kata husika,
10. Kusimamia sheria na kanuni za Mifugo na Uvuvi
MALENGO YA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Lengo kubwa ni kuhakikisha wafugaji wanapata Elimu ya ufugaji bora wa kisasa na wenye tija kwa nia ya kumfanya mfugaji aongeze kipato ili aondokane na umaskini uliokithiri lakini pia kuongeza pato la Taifa.
VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.