Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2017-2018.pdf
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
WILAYA YA MISUNGWI
TAARIFA FUPI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA MHE, DR.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
DESEMBA, 2016.
Imeandaliwa na:
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,
MISUNGWI
YALIYOMO
Jedwali Na.1: ENEO LA WILAYA KIUTAWALA NA SHUGHULI ZA WANANCHI. 5
1.0 Hali ya Ulinzi na Usalama. 6
3.0 Mapato Ya Ndani ya Vyanzo vya Halmashauri Kwa mwaka 2016/2017. 6
3.1UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI KWA HALMASHAURI. 6
3.1.2 Mikakati ya ukusanyaji wa Mapato. 7
3.2 Ruzuku toka Serikali Kuu.. 8
5.1 Matumizi ya zana za kilimo. 9
5.3.1 Pembejeo za Kilimo zenye Ruzuku ya Serikali: 10
Jedwali Na.5: Usambazaji wa Mbegu bora. 11
5.4 Hali ya Kilimo na Chakula. 11
5.5 Mafanikio katika Sekta ya Kilimo: 13
5.6 Changamoto katika Sekta ya Kilimo: 13
5.7Mikakati ya kukabiliana na changamoto. 14
10.0 HIFADHI YA MAZINGIRA NA MISITU: 18
11.0 SEKTA YA MADINI NA NISHATI. 19
11.2 Hali ya Umeme Wilayani: 19
13.2 Hali ya Uwekezaji na Uwezeshaji Wilayani: 20
13.3 Mikakati ya Halmashauri ya Wilaya kuhusu EPZ.. 21
14.0SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII. 21
15.0 SEKTA YA MIUNDOMBINU.. 22
15.1 SEKTA YA MIUNDO MBINU.. 22
15.2 Hali ya barabara wilayani 22
15.4 Jinsi ya kukabili changamoto. 23
16.2 Idadi ya walimu katika Shule za Msingi hadi desemba 2016 2016: 26
16.2.1 Idadi ya walimu na upungufu: 26
17.1 CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA SEKTA YA ELIMU WILAYANI: 29
17.2 MIKAKATI YA UBORESHAJI WA ELIMU: 29
18.2 AFYA YA UZAZI NA MTOTO: 30
18.5UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA VYA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA: 31
18.6 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA WILAYANI: 32
18.7 Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto: 32
19.3 MAPAMBANO DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO: 33
19.4 WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI: 33
21.1.1 TAARIFA YA HALI HALISI YA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI MJINI MISUNGWI. 34
21.2 Usambazaji wa maji Mjini (Mitindo Water Supply): 34
21.5 Namna ya kutatua changamoto hizi (The wayforward). 35
22.1 MIRADI YA MAENDELEO PROGRAMU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI (RWSSP) 36
22.2 Mchanganuo wa Miradi ya maendeleo;-. 36
22.3 Hali ya utekelezaji kufikia Septemba 30 2016 ni kama ifuatavyo:-. 36
22.4 Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Ngaya hadi Matale. 37
22.5 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo. 37
22.6 Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba wa Matale –Manawa-Misasi. 37
22.7 Hali ya utekelezaji kwa sasa ni kama ifuatavyo:-. 37
22.8 Changamoto za Idara katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo. 38
22.9 Utatuzi wa Changamoto. 38
23. 0 HALI YA UTUMISHI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.. 39
23.3 CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA UTUMISHI: 39
23.4 TAARIFA YA UHAKIKI WA WATUMISHI. 40
24.0 Huduma za Fedha Zinazotolewa na Taasisi mbalimbali 40
TAARIFA FUPI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA MHE, DR.JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI, RAIS YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA.
DESEMBA, 2016.
UTANGULIZI
Mwaka wa kuanzishwa Wilaya
|
1995 |
Eneo:
Eneo la Wilaya kwa ujumla (Km2) |
2,553 |
Eneo kavu (Km za mraba)
|
2,378 |
Eneo la Maji (Km za mraba)
|
175 |
Mahali Wilaya ilipo:
Latitude Kusini mwa Ikweta |
2º 35’ na 3 º15’ |
Longitude Mashariki mwa Greenwich
|
33º 15' |
Hali ya hewa:
Hali ya joto liko kati ya nyuzi |
25°C na 30°C |
Hali ya mvua (mm)
|
500 – 700 |
Mvua za vuli na masika hunyesha kati ya miezi ya
|
Okt – Des, Machi – Mei |
Idadi ya watu:
Watu wote |
351,607 |
Wanaume
|
173,997 |
Wanawake
|
177,610 |
Ongezeko la watu kwa mwaka
|
2.8% |
Idadi ya Kaya
|
54,093 |
Idadi ya watu kwa kila kaya
|
6.5 |
Mgawanyo wa kiutawala:
|
|
Idadi ya Majimbo ya uchaguzi
|
1 |
Tarafa
|
4 |
Kata
|
27 |
Vijiji
|
113 |
Vitongoji
|
724 |
Idadi ya shule za msingi
|
Shule binafsi 7
|
Shule za serikali 138
|
|
Idadi ya shule za sekondari
|
Shule binafsi 4
|
Shule za serikali 23
|
|
Idadi ya vituo vya afya
|
4
|
Idadi ya zahanati
|
Zahanati za binafsi 2
|
Zahanati za serikali 38
|
|
Idadi ya Hospitali
|
Hospitali ya binafsi 1
|
|
Hospitali ya Serikali 1
|
“Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni kuwa na Maisha bora kwa watu wake kwa kuwapatia huduma endelevu za kijamii na kiuchumi kwa misingi ya utawala bora.”
“Dhima ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni kuhakikisha kuwa jamii na wadau wote wanashiriki kikamilifu katika kupata huduma endelevu za kiuchumi na kijamii kwa kutumia rasilimali na mazingira yaliyopo yakiwemo ya utawala bora.”
Hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya kuwepo kwa matukio ya uvunjifu wa amani yanayojitokeza mara kwa mara.
Hali ya kisiasa wilayani kwa ujumla ni shwari, uhusiano kati ya vyama vya siasa vilivyopo na Serikali ni mzuri. Hali hii imewezesha shughuli za maendeleo kutekelezwa vizuri.
Katika Mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha shilingi 1,601,368,000.00 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani.Hadi kufikia tarehe 30 Novemba, 2016,Halmashauri imeshakusanya jumla ya shilingi 499,413,128.42 ambayo sawa na asilimia 31.19 .Hata hivyo Halmashauri ipo nyuma kwa asilimia 9.8 katika makusanyo kutokana na kutoletewa kwa gawio asilimia 30 kutoka wizara ya ardhi ambacho ni chanzo kimojawapo, kodi ya majengo bado haijaanza kukusanywa kutokana na kwamba Halmashauri bado ipo katika maandalizi ya kisheria.Vyanzo vikuu vya mapato ya ndani kwa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ni ushuru wa kokoto na mchanga, ushuru wa stendi ,ushuru wa magulio , minada ya mifugo, kodi ya ardhi,kodi ya majengo na ushuru wa huduma.
Kuiomba serikali iangalie upya swala la ulipaji wa ushuru wa huduma (service levy) kwani makampuni yanayofanya kazi hapa hususani makampuni ya uchimbaji kokoto na mengine yamekuwa yakilipia ushuru katika makao makuu ya ofisi zao yaliyopo jijini Mwanza na wakati shughuli hizo zinafanyika katika wilaya ya Misungwi.
Kuna sheria ambazo zimepitwa na wakati. Aidha kuanza mchakato wa utungaji wa sheria ndogo ili kuongeza mapato.
Kuomba serikali iongeze safari za magari madogomadogo ya abiria toka Mwanza mjini hadi Nyashishi ambapo tuna eneo la stendi, lakini halifanyi kazi kutokana na kukosekana kwa route hiyo.
Uboreshaji wa Takwimu za vyanzo mbalimbali vya mapato.
Kuboresha Ushikiano wa Wadau, Maafisa Watendaji wa Kata na Waheshimiwa Madiwani katika ukusanyaji wa mapato.
Kubaini vyanzo vipya vya mapato ambavyo bado havijafikiwa kutoka ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji hii ni pamoja na kuandaa rejista za ukusanyaji wa mapato kwa kila chanzo kilichopo kwenye kata.
Jeshi la polisi kushirikishwa ipasavyo ili kusaidia ukusanyaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya Halamshauri
Kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau, watendaji, na waheshimiwa Madiwani ili kuwa na ukusanyaji wenye tija (Team work), Aidha wadau kama TRA , Madini na TMAA kutoa takwimu zitakazosaidia ukadiriaji wa vyanzo mbalimbali vya mapato
Watumishi na wakala wanaohusika katika ukusanyaji wa mapato kujengewa dhana ya uaminifu kwa wakusanyaji wa mapato.
Uboreshaji na uanazishaji wa huduma za msingi kwa wananchi ikiwemo magulio ya Halamshauri na vyanzo vingine ili kuchangia hali ya wananchi kuotoa tozo mbalimbali za Halamshauri
Ubunifu katika kukusanya mapato, ambao utaruhusu wadau mbalimbali kufanya uboreshaji katika maeneo mbalimbali.
Kuwatumia watendaji wa kata na vijiji vizuri kudhibiti mianya ya utoroshaji wa mazao hasa wale wanaoficha mazao katika miji ya watu. Yule atakayekamatwa anaficha mazao alipie asilimia fulani kama adhabu.
Wafanyabiashara waandikishwe na kuorodheshwa ili kila mmoja awajibike kulipa kodi. Kazi hii ifanywe na watendaji wa kata na vijiji
Ujenzi wa choo katika gulio la Mabuki
Mashine za EFD /POS kutotumika kwa ukamilifu, hivyo elimu izidi kutolewa juu ya suala zima la uaminifu.
Kutoa kipaumbele katika ulipaji wa Kodi ya majengo na ardhi ili iweze kulipwa ipasavyo
Kuboresha sheria ndogo zilizopitwa na wakati hasa za ukusanyaji wa mapato ili tuweze kuboresha Halmashauri yetu .
Katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri ya wilaya imepanga kutumia kiasi cha Tshs.
10, 861,714,709.18 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Ardhi, Ujenzi, Mipango, Kilimo/Mifugo na Utawala.Fedha hizo zitatoka katika vyanzo mbalimbali navyo ni Serikali Kuu, Halmashauri ya Wilaya, Busket Fund, NRWSSP, Mfuko wa Jimbo, SEDP, TASAF, TACAIDS, Road Fund, LGCDG na michango ya jamii.
Hadi kufikia tarehe 30 Novemba 2016, Halmashauri ya wilaya imepokea jumla ya kiasi cha Tshs 2,385,720,866 za miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 23.50 .Fedha hizi zimetolewa na vyanzo mbalimbali ambavyo ni serilkali kuu,LGCDG, na TASAF kwa mchanganuo ufuatao: kiasi cha Tshs 300,000,000 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi ambazo ni Mitindo,Busagara na Misungwi (Shule maalumu) kutoka Serikali kuu,imepokea Tshs. 368,700,000 kwa ajili ya kuboresha elimu ya msingi pia toka serikali kuu.Sambamba na hilo halmashauri imepokea Tshs 221,565,000 toka LGCDG,imepokea Tshs 23,917,000.00 za mfuko wa jimbo, imepokea tshs 1,255,351,500 .00 toka TASAF,imepokea Tsh 216,187,183.16 za miradi wa sekta ya maji vijijini. Hata hivyo kiasi cha Tshs.1,034,834,500.00 kimetumika ambayo ni sawa na asilimia 43.37% ya fedha zilizopokelewa hadi sasa.
Pato la wananchi kiwilaya limekuwa likiongezeka kwa asilimia tano na kinachochangia kuongezeka huko ni uwepo wa shughuli za kilimo, wachimbaji wadogowadogo wa madini, uvuvi, ufugaji, shughuli za biashara na taasisi za umma. Kwa mwaka 2012 pato la mwananchi mmoja mmoja wa Wilaya ya Misungwi linakadiriwa kufikia 647,777.00 kwa mwaka na hivyo kufanya Pato la wilaya kuwa shilingi 455,103,461.00 (Sensa ya mwaka 2012.)
Jedwali Na.2: Matumizi ya Zana za Kilimo
Wilaya/Halmashauri |
Idadi ya matrekta |
Asilimia ya wakulima wadogo wanaolimia matrekta |
Idadi ya plau |
Asilimia ya wakulima wanaotumia plau |
Idadi ya wakulima wanaotumia jembe la mkono |
% |
P.Tiller |
% |
Misungwi
|
119
|
8
|
5,730
|
43
|
202788
|
47
|
48
|
2
|
Jumla
|
119
|
8
|
5,730
|
43
|
135,825
|
47
|
48
|
2
|
Halmashauri ya Wilaya ina eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji lenye ukubwa wa Ha 8,969.Aidha Halmashauri ya Wilaya inazo skimu 6 za kilimo cha umwagiliaji zenye ukubwa wa Ha. 2,975.Ambapo Skimu 3 zinalimwa na kumwagilia nazo ni Igongwa yenye Ha 240 zinazomwagilia,Ilujamate yenye Ha 75 zinazomwagilia ,Nyashidala Ha 220 zinazomwagilia na skimu 3 hazifanyi kazi nazo ni Nyambeho yenye Ha 200 ambayo miundombinu yake iliondolewa na mafuriko y mwaka 2006, Igenge yenye Ha 200 Mradi haujakamilika na umesimama muda mrefu na Mbarika yenye Ha 200 ulisimama.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
5.2.1 Changamoto umwagiliaji
Wilaya ya Misungwi haikupata mgao wowote wa Pembejeo zenye Ruzuku ya Serikali (Mbolea na Mbegu), isipokuwa wakulima wananunua kwenye maduka ya pembejeo ya wafanya biashara binafsi.
Jedwali Na.4: Mbolea iliyonunuliwa na wakulima mwaka 2013/14 hadi 2016/17 (TANI)
Namba |
Aina |
2013/2014 |
2014/2015 |
2015/2016 |
2016/2017 |
1
|
UREA
|
57 |
65 |
73 |
98 |
2
|
CAN
|
60 |
64 |
76 |
82 |
3
|
S/A
|
0 |
0 |
0 |
0 |
4
|
NPK
|
23 |
28 |
33 |
41 |
5
|
MINJINGU
|
0 |
0 |
0 |
0 |
JUMLA
|
140 |
157 |
182 |
221 |
Namba
|
Aina
|
2013/2014 |
2014/15 |
2015/2016 |
2016/2017 |
1
|
Pamba
|
88.012 |
192 |
195 |
315.05 |
2
|
Mahindi
|
31 |
39 |
45 |
57 |
3
|
Mpunga
|
0 |
0 |
0 |
0 |
4
|
Mtama
|
0.570 |
0.530 |
0.410 |
0.113 |
5
|
Alizeti
|
0 |
0 |
0 |
6 |
6
|
Bustani
|
1.5 |
2 |
2.5 |
3.2 |
JUMLA
|
121.082 |
233.530 |
242.910 |
381.363 |
Wilaya imehamasisha wakulima kujiunga na kilimo cha mkataba cha pamba ili waweze kukopeshwa pembejeo. Jumla ya tani 315.05 za mbegu ya pamba zimesambazwa vijijini ambapo jumla ya tani 168.12 zimekopeshwa kwa wakulima. Hata hivyo kutokana na upungufu wa mvua, wakulima wengi hawajapanda mbegu hizo.
5.3.3 Zao la Alizeti
Ili kuhamasisha kilimo cha alizeti, wilaya imenunua jumla ya tani 6 za mbegu ya alizeti, mbegu hizo zimesambazwa kwa wakulima. Baada ya mavuno kila mkulima atarudisha kiasi cha mbegu alichopewa ili na wakulima wengine waweze kupewa mbegu hizo.
Wilaya ya Misungwi imekuwa ikijishughulisha na kilimo katika maeneo mbalimbali ingawa hali ya hewa na mwenendo wa mvua si wa kuridhisha. Hali halisi ya utekelezaji katika sekta hii ikihusisha eneo la kilimo, matumizi ya zana za kilimo na ununuzi wa matrekta.
Chakula aina ya Nafaka ( Mahindi, Mpunga, na mtama na mawele ), vyakula vya mizizi ( Mihogo na viazi vitamu vibichi ) pamoja na vyakula aina ya mikunde vinapatikana katika masoko na magulio yaliyomo wilayani. Vyanzo vya upatikanaji wa mazao hayo ya chakula ni kutoka ndani ya wilaya na kiasi kidogo kutoka nje ya wilaya hasa kwa zao la mikunde aina ya maharage ndizi za kupika na mbivu, viazi mviringo, unga wa ngano na Matunda aina ya nanasi.
Jedwali Na.6: MAHITAJI YA CHAKULA KWA MWAKA 2016 / 2017.
Idadi ya watu
|
Aina ya chakula
|
Mahitaji kwa mwaka
|
Uzalishaji
2015 / 2016 |
Upungufu / Ziada
( Tani ) |
Maelezo
|
(Sensa ya 2012) 326,503
|
Nafaka ( wanga )
|
89,380
|
100,989.30
|
+ 11,609.3
|
Januari 2017 kutakuwa na upungufu wa chakula kwa sababu mazao yaliyopandwa mwezi Octoba hayakupata mvua za kutosha, hivyo mavuno ya mazao hayo yatakuwa kidogo na kusababisha upungufu wa chakula.
|
Mikunde ( Protini )
|
8,938
|
9,250.1
|
+ 312.1
|
5.5.2 Mikakati ya kukabiliana na hali ya chakula
5.5.3 BEI YA VYAKULA KUISHIA NOVEMBA, 2016
Bei ya vyakula mbalimbali (vyakula aina ya nafaka, mizizi na mikunde vinapatikana na kuuzwa katika masoko na magulio wilayani kwa bei ya kutofautiana kati ya soko na soko/ gulio na gulio.
Jedwali Na 7: Jedwali lifuatalo hapo chini linaonyesha wastani wa bei ya vyakula kuishia Novemba, 2016
Aina ya chakula |
Upatikanaji wake |
MAELEZO / AINA YA KIPIMO |
||
Ndani ya Wilaya |
Nje ya Wilaya |
Novemba
2016 |
|
|
Mahindi ⃰
|
√ |
√ |
12,000/- |
Kwa Ndoo ya kilo 20
|
Mtama
|
√ |
0 |
9,900/- |
Kwa Ndoo
|
Uwele
|
√ |
0 |
9,900/- |
Kwa Ndoo
|
Mpunga
|
√ |
0 |
9,900/- |
Kwa Ndoo
|
Mchele ⃰
|
√ |
0 |
1,200/- |
Kwa Kg.
|
Muhogo( udaga)
|
√ |
0 |
8,000/- |
Kwa Ndoo
|
Viazi vitamu- vibichi
|
√ |
0 |
500/- |
Kwa kg
|
Viazi vitamu- vikavu
|
√ |
0 |
700/- |
Kwa kg
|
Choroko
|
√ |
0 |
2000/- |
Kwa kg
|
Maharage ⃰
|
√ |
√ |
2,000/- |
Kwa Kg
|
Dengu
|
√ |
0 |
2000/- |
Kwa kilo
|
Karanga(menywa)
|
√ |
√ |
2,500/- |
Kwa kilo
|
Karanga ( maganda)
|
√ |
0 |
9,000/- |
Kwa Ndoo
|
Njugumawe
|
√ |
√ |
3,000/- |
Kwa kg.
|
Kunde
|
√ |
0 |
1,600/- |
Kwa kg
|
Viazi Mviringo
|
0 |
√ |
1,000/- |
Kwa kg
|
Ndizi za Kupika
|
0 |
√ |
1,200/- |
Kwa kg
|
* Chakula kikuu
5.4 MALENGO YA KILIMO MSIMU 2016/17
Jedwali Na.8: Kilimo cha Mazao ya chakula na Biashara : Wilaya msimu huu imeweka Malengo ya kilimo katika msimu huu 2016/17. Malengo hayo ni kama ifuatavyo:-
Asilimia 70 ya wakulima wote wamehamasika kutumia pembejeo (madawa na mbolea) pamoja na kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.
Wakulima wamehamasika kununua zana za kilimo kama vile Trekta kubwa na ndogo kwa kupitia njia ya mikopo.
Wakulima, vikundi na taasisi wamehamasika kulima mazao ya pamba na alizeti.
Mvua zinazonyesha msimu huu wa vuli siyo za kuridhisha hivyo kutakuwepo na upungufu wa mavuno.
Bei za mazao ya mazao ya chakula hasa mahindi imepanda toka Tsh. 12,000 mwezi Novemba 2016 hadi Tsh. 16,000 mwezi Desemba kwa debe la kilo 20.
Kuwaelimisha wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji.
Kuhakikisha kila kaya inajitosheleza kwa chakula na kupata ziada kwa ajili ya kuuza, pia kuwahimiza wakulima kulima mazao yanayostahimili ukame angalau kila kaya kulima ekari moja ya mtama/uwele au mihogo.
Kuhamasisha jamii kupanda miti ambayo ni rafiki kwa mazingira, hii itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kuunganisha wakulima na tasisi mbalimbali zinazokopesha zana za kilimo hususani matrekta.
Kuwawezesha wakulima kupima mashamba yao ili kupata hati miliki za kimila ambazo zitawawezesha kukopa.
Wilaya ina jumla ya eneo la Ha. 96,000 ambalo linafaa kwa malisho ya mifugo. Idadi ya mifugo iliyopo ni 175,708 idadi hii inajumuisha Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo. Hata hivyo maeneo mengi hayafai kwa ufugaji kutokana na kuwepo na ukosefu wa maji hasa wakati wa kiangazi. Wilaya inaendelea kutoa elimu ya kutumia madume bora na uhamilishaji ili kupata mifugo michache yenye tija kwa lengo la kujaribu kuwatoa katika kundi la uchungaji kuwa wafugaji, vilevile elimu ya upandaji na hifadhi ya malisho hutolewa mara kwa mara. Aidha wananchi wamekuwa wakihimizwa kuogesha mifugo yao ili kuepukana na magonjwa ya mifugo na chanjo hutolewa kudhibiti magonjwa ya milipuko na kuambukiza
Jedwali Na 9: IDADI YA MIFUGO WILAYANI
Wilaya |
Idadi ya mifugo |
|
|
|
|
Eneo linalotumika kwa malisho (Ha) |
Uwezo wa malisho (carrying capacity) |
||
Ng’ombe
|
Mbuzi
|
Kondoo
|
Mbwa |
Nguruwe |
Punda |
Kuku |
|||
Misungwi
|
131,250
|
34,214
|
10,224
|
10,336
|
942
|
801
|
194,556
|
96,000
|
1.966
|
Jumla
|
131,250
|
34,214
|
10,244
|
10,336
|
942
|
801
|
194,556
|
96,000
|
1.966
|
Ili kupambana na umaskini wananchi wanaelimishwa na kuhimizwa kujiunga katika vikundi ili kukusanya nguvu na kutatua matatizo yanayowakabili katika uzalishaji na masoko. Katika jitihada hizo Wilaya ya Misungwi imekuwa na jumla ya vyama vya ushirika 144 vya aina mbalimbali. Aina ya vyama vilivyopo ni SACCOs (Savings and Credit Co operatve Society) 89, AMCOs (Agricultural Marketing Co operative Socities) 40, ushirika aina nyingine viko 15 VICOBA (Village Community Banks) viko 30, pia kuna aina nyingine ya vyama.
Vilevile Wilaya imeweka mkazo zaidi katika vyama vya Akiba na Mikopo na ambapo jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi 2.4 bilioni tayari imeshakopeshwa kwa wanachama wake.
Jedwali Na.10: IDADI YA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA WILAYA HADI NOVEMBA 30, 2016
Aina ya Chama |
Misungwi |
Jumla |
Vyama vya mazao (AMCOS)
|
40 |
40 |
SACCOS
|
89 |
89 |
Usafirishaji
|
1 |
1 |
Huduma
|
- |
- |
Maduka
|
0 |
0 |
Viwanda
|
4 |
4 |
Ushirika Shughuli Nyingi
|
0 |
0 |
Uvuvi/samaki
|
4 |
4 |
Nyumba
|
0 |
0 |
Ujenzi
|
1 |
1 |
Madini
|
1 |
1 |
Umwagiliaji
|
4 |
4 |
Vyama vinginevyo
|
0 |
0 |
Vyama vikuu
|
0 |
0 |
Jumla
|
144 |
144 |
|
Jedwali Na.11: HALI YA VYAMA VYA USHIRIKA VYA AKIBA NA MKOPO (SACCOS) KUISHIA TAREHE 30 NOVEMBA, 2016
HALMASHAURI |
IDADI YA |
MTAJI |
MIKOPO |
||||||
SACCOS |
WANACHAMA |
HISA |
AKIBA |
AMANA |
JUMLA |
TOLEWA |
REJESHWA |
BAKI |
|
Misungwi
|
89
|
91,125
|
288,100,010
|
194,800,347
|
85,000,800
|
567,901,157
|
2,400,906,600
|
960,540,000
|
1,440,360,600
|
Jumla
|
89
|
91,125
|
288,100,010
|
194,800,347
|
85,000,800
|
567,901,157
|
2,400,906,600
|
960,540,000
|
1,440,360,600
|
Halmashauri ya Wilaya inashirikiana na TCCIA ili kuimarisha biashara katika sekta binafsi.
Aidha wakulima na wafanya biashara wilayani wanashiriki katika mashindano ya nane nane pamoja na soko la Afrika Mashariki yanayofanyika kimkoa na Kitaifa na kimataifa kila mwaka kuonyesha bidhaa zao ili kupanua soko.
Elimu ya utaratibu wa uanzishaji wa Biashara inatolewa kwa wafanyabiashara kila mwaka ili kufanikisha urasimishaji wa Biashara kwa utoaji wa Leseni za Biashara. Elimu hii hutolewa kwa Umma kwa kutumia vipeperushi na matangazo kwa kutumia vipaza sauti.
Wilaya imetenga eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa Hekta 2400 katika vijiji vya Nyang’homango na Mwasonge Tarafa ya Usagara, pia Halmashauri ya Wilaya imetenga ekari 83 eneo la Somanda Misungwi mjini kwa ajili ya maendeleo ya viwanda.
Jumla ya vikundi vitatu (3) vya usindikaji vimepatiwa mafunzo navyo ni Nyota Group cha maziwa na ngozi, Inonelwa cha kusindika ngozi na Alovera Upendo cha Mabuki kinachosindika mvinyo. Aidha wajasiriamali wanaozalisha viazi Carrot wameunganishwa na makampuni makubwa yanayotengeneza biscuits.
Wilaya ya Misungwi ina eneo lenye kilomita za mraba 175 ambapo lipo ndani ya ziwa victoria. Eneo hilo la ziwa lina jumla ya wavuvi 1,369 na mitumbwi 345 kwa takwimu za mwaka 2014 . Wadau wa uvuvi 281walipata elimu juu ya uvuvi wa kisasa katika vijiji vya kandokando ya ziwa. Vikundi 10 vya uvuvi shirikishi yaani (Beach Management Units) BMU vinaendelea kuimarishwa.
Katika kipindi cha miaka mitano (2012- 2016) jumla ya mabwawa ya kufugia samaki 101 yamechimbwa katika vijiji vya Mwaniko (4), Mbarika (14), Kigongo (13), Ilalambogo (6), Lugobe (6), Mwalogwabagole (26), Mwajombo (12), Nyang’homango (6), Misungwi (4), Sawenge (4),Magaka (2) na Nyamatala (4).
Uvunaji wa samaki umekuwa ukipungua kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2016 hii ni kutokana na jitihada zinazofanywa na wilaya za kuhakikisha kuwa uvuvi haramu unakomeshwa, kabla ya jitihada za kukomesha uvuvi haramu takwimu zilikuwa juu sana kwakuwa hata wale samaki ambao hawakutakiwa kuvunwa walikuwa wanahesabiwa, mabadiliko ya hali ya hewa, kupungua kwa kina cha maji ziwani, kilimo cha kandokando ya ziwa na matumizi mabaya ya dawa za kilimo na mifugo. Aidha eneo la Ziwa Victoria lililopo upande wa Misungwi ni maalum kwa ajili ya uzalishaji samaki (Breading site) hivyo shughuli za uvuvi zinasimama kipindi cha mwezi Januari hadi Juni yaani ziwa hufungwa.
Maeneo yanayostahili kuhifadhiwa yapo, mfano misitu ya hifadhi ambayo ipo chini ya Halmashauri (Local authority forestry reserves) ambazo ni Mamani km za mraba 758, sisu km za mraba 921, malenge km za mraba 220 na Ilangafipa km za mraba 1,336. Hata hivyo ukubwa wa eneo uliooneshwa ni wa hapo awali na umepungua kutokana na uchomaji ovyo, ukataji wa miti, upanuzi wa makazi, ufugaji na kilimo na Uchimbaji wa Dhahabu.
Vijiji vilivyopo katika mpango wa usimamizi shirikishi wa mazingira ni vile vilivyo na hifadhi za uoto wa asili, taasisi na shule. Wastani wa upandaji miti kwa kwa mwaka ni miti 1,008,900 na miti inayostawi ni wastani wa miti 898,213
Wilaya |
2013/2014 |
2014/2015 |
2015/2016 |
2016/17 |
Misungwi
|
634,700
|
897410
|
1,276,189
|
1,300,00,000
|
JUMLA
|
634,700
|
897410
|
1,276,189
|
|
Wilaya ya Misungwi ina maeneo yenye madini ya Dhahabu ambapo wachimbaji wadogo zaidi ya 400 wamekuwa wakijihusisha na uchimbaji wa madini hayo katika maeneo ya Ishokera na Mwamazengo. Pia Wilaya ina madini ya Almasi katika kijiji cha Mwanangwa.Aidha Wilaya ina makampuni yanayoponda kokoto na maeneo ya mchanga katika kijiji cha Nyang’homango, Isamilo, Mwasonge, Fella, Ntende na Usagara
Hata hivyo Halmashauri inaendelea kuhamasisha wachimbaji wadogo wadogo kuunda na kusajiri vikundi vya uchimbaji ili waweze kupata mikopo katika taasisi za kifedha
Wilaya imeunganishwa na umeme wa Grid ya Taifa (Tanesco). Umeme huu unapatikana katika miji ya Misungwi, Usagara, Bukumbi, Misasi na Koromije. Hata hivyo vijiji mbalimbali vimepata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini (Rural Electrification Agency – REA) na Electricity 5.
Kwa sasa Halmashauri inatarajia kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ili kuendelea na utekelezaji wa azma hiyo. Jedwali lifuatalo linaonesha mchanganuo wa mizinga nyuki Wilayani.
Jedwali Na.13: Mchanganuo wa Mizinga ya nyuki Wilayani
Aina ya Mizinga ya Nyuki |
Idadi |
Wamiliki |
Mizunga ya asili
|
400
|
Watu binafsi
|
Mizinga ya kisasa kabla ya maelekezo ya Dododma
|
130
|
Watu binafsi na kikundi kimoja
|
Mizinga ya kisasa baada ya maelekezo ya Dodoma kufikia leo
|
1715
|
|
Jumla kuu
|
2245
|
|
Halmashauri ya wilaya ina masjala za ardhi 3 zilizokamilika na zinatoa huduma katika vijiji vya Kasololo, Isamilo na Matale. Masjala za Kasololo na Matale zilipata fedha kwa ajili ya kuandaa matumizi bora ya ardhi kupitia mradi wa MKURABITA na Idadi ya mashamba yaliyopimwa kupitia MKURABITA ni 1,341 kwa vijiji vyote viwili, katika kijiji cha Kasololo mashamba 863 yalipimwa na Matale mashamba 478 yalipimwa na mashamba 548 yameshaingizwa katika kompyuta kwa hatua ya uandaaji wa Hati. Mpaka sasa idadi ya Hati zilizoandaliwa ni 793 ikiwa Hati 474 ni za kijiji cha Kasololo na Hati 319 ni za kijiji cha Matale.
Aidha Wilaya inaendelea kuhamasisha wananchi kuweza kupimiwa maeneo yao ili kuweza kupata Hati miliki zitakazo wawezesha kupata utambulisho na udhamini katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Halmashauri ya wilaya ya Misungwi imeunda kitengo cha uwekezaji chenye waatalamu 3.Ambapo walishajengewa uwezo na wataalamu wa EPZA. Halmashauri imeshatenga eneo la uwekezaji katika kata za Ukiruguru na Bulemeji. Ukubwa wa eneo lililotengwa kwa matumizi ya mradi huu wa EPZ ni takribani hekta 2,400.Hata hivyo uhamasishaji umefanyika kwenye maeneo haya, Watendaji wa Halmashauri na wajumbe wa kamati ya fedha wamejengewa uwezo juu uwekezaji wa viwanda na wataalmu kutoka EPZA.
Mikakati ya Halmashauri ya Wilaya kuhusu eneo la EPZ ni kama ifuatayo:-
Kwa kuwa maeneo haya yameendelea kuendelezwa na wananchi, Halmashauri inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipia fidia kwa awamu.
Timu hii ya uhamasishaji iliweza kufanya vikao vyake na kuwaeleza wananchi nia ya Serikali kutwaa ardhi ya kijiji kuwa chini ya kamishna kwa manufaa ya umma na jinsi wananchi hao watakavyo faidika kutokana na mradi huo wa EPZ kabla na baada kutwaa ardhi hiyo.
Vijiji ambavyo vipo kwenye eneo la mradi uwekezaji wa viwanda villikubaliana na mradi huo wa EPZ na kuomba haki zao za msingi zipatikane kwa muda muafaka na mhatasari huo uliwasilishwa ofisi ya ardhi wilaya.
Mtandao wa barabara umegawanyika katika sehemu kuu mbili, nazo ni
Mtandao wa barabara Wilayani zilizo chini ya Mkoa, ambazo zipo katika mafungu mawili;-
Barabara za Taifa (Trunk Roads) - 53 Km
Barabara ya Mkoa (Region Roads) - 167 Km
Jumla - 220 Km
(b) Mtandao wa barabara zilizo chini ya Halmashauri nazo ziko mafungu mawili;-
Jumla kuu barabara zote ni - 704 Km
Hali ya barabara zilizo chini ya Halmashauri tangu Januari 2006 hadi June 2016 ni kama ifuatavyo:-
Changamoto iliyopo kubwa ni ya uhaba wa fedha kulingana na mahitaji halisi. Hii imesababisha;
Tumeweza kuomba fedha za nyongeza nje ya bajeti toka mfuko wa barabara.
Jedwali Na.14: MGAWO WA FEDHA ZA BARABARA 2014/2015 NA 2015/2016 NA 2016/2017:
TAASISI |
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2014/ 2015 (Tshs: )
|
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2015/ 2016 (Tshs: )
|
BAJETI YA FEDHA ZA BARABARA 2016/ 2017 (Tshs: )
|
JUMLA |
Misungwi
|
914,300,000
|
391,300,000
|
882,220,000
|
2,187820,000
|
JUMLA KUU
|
914,300,000
|
391,300,000
|
882,220,000
|
2,187820,000
|
Wilaya ya Misungwi haina miundo mbinu ya vivuko inavyovisimamia, kivuko kilichopo kinasimamiwa na mamlaka nyingine ambayo ni TEMESA
Jedwali Na.15: IDADI YA SHULE ZA AWALI NA MSINGI – KIWILAYA, 2016:
WILAYA
|
SHULE ZA AWALI
|
SHULE ZA MSINGI
|
||||
Serikali
|
Binafsi
|
Jumla
|
Serikali
|
Binafsi
|
Jumla
|
|
Misungwi
|
138
|
7
|
145
|
138
|
7
|
145
|
JUMLA
|
138
|
7
|
145
|
138
|
7
|
145
|
Jedwali Na.16 : IDADI YA SHULE ZA MSINGI NA WANAFUNZI: 2016
AWALI – DARASA LA KWANZA
Na
|
WILAYA
|
IDADI YA SHULE
|
IDADI YA WANAFUNZI
|
||||
Serikali
|
Binafsi
|
Jumla
|
Wav
|
Was
|
Jumla
|
||
1
|
Misungwi
|
138
|
7
|
145
|
42,949
|
34,525
|
67,474
|
|
JUMLA
|
138
|
7
|
145
|
42,949
|
34,525
|
67,474
|
Jedwali Na.17: Uandikishaji wa Darasa la Kwanza 2016:
NA |
WILAYA |
IDADI YA WANAFUNZI |
||
WAV |
WAS |
JUMLA |
||
1
|
Misungwi
|
9,590 |
9,264 |
18,854 |
|
JUMLA
|
9,590 |
9,264 |
18,854 |
Jedwali Na.18: IDADI YA WANAFUNZI DARASA LA I HADI VII - 2016
NA |
WILAYA |
IDADI YA WANAFUNZI
|
|||
|
WAV
|
WAS
|
JUML
|
||
4 |
Misungwi |
Serikali
|
35,977 |
37,463 |
73,440 |
|
|
Binafsi
|
524 |
513 |
1,037 |
|
JUMLA |
|
36,501 |
37,976 |
74,477 |
Jedwali Na.19: TAKWIMU ZA WATAHINIWA WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2015 NA 2016 NA KUFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2016 NA 2017 WILAYA YA MISUNGWI, MKOA WA MWANZA
|
|
||||||||||
NA
|
MWAKA
|
WALIOFANYA |
WALIOFAULU |
||||||||
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
%
|
WAS
|
%
|
JML
|
%
|
|||
1
|
2015
|
2,474 |
2,921 |
5,395 |
1,991 |
80 |
2,199 |
75.3 |
4,190 |
77.7 |
|
2
|
2016
|
2,801 |
3,291 |
6,092 |
2,118 |
75.64 |
2064 |
62.71 |
4,182 |
68.65 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Jedwali Na. 20: SAMANI ZA SHULE ZA MSINGI HADI DESEMBA 2016
WILAYA
|
MADAWATI |
MEZA ZA WALIMU |
VITI VYA WALIMU
|
KABATI ZA WALIMU |
||||||||
MISUNGWI
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu/Ziada
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
JUMLA
|
34,597
|
35,132
|
535
|
3,178
|
1,087
|
2,091
|
3,504
|
1,366
|
2,138
|
1,906
|
411
|
1,495
|
Jedwali Na.21: MAHITAJI YA WALIMU HADI DESEMBA 2016
|
||||
NA |
WILAYA |
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
3
|
Misungwi
|
2,298
|
1,492
|
806
|
|
JUMLA
|
2,298
|
1,492
|
806
|
Jedwali Na.22: MAHITAJI YA MAJENGO YALIYOPO NA UPUNGUFU KATIKA SHULE ZA MSINGI: HADI DESEMBA 2016
WILAYA |
MADARASA |
NYUMBA ZA WALIMU |
VYOO |
||||||
MAH |
YAL |
UPUNGUFU |
MAH |
ZILI |
UPUNGUFU |
MAH |
YAL |
UP |
|
Misungwi
|
1,921
|
1,045
|
876
|
1,558
|
377
|
1,181
|
3,445
|
1,129
|
2,316
|
JUMLA
|
1,921
|
1,045
|
876
|
1,558
|
377
|
1,181
|
3,445
|
1,129
|
2,316
|
Jedwali Na.23: IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI ZENYE KIDATO CHA I-IV HADI DESEMBA 2016
|
|||
WILAYA
|
SERIKALI
|
ZISIZO ZA SERIKALI
|
JUMLA
|
Misungwi
|
23 |
04 |
27 |
JUMLA
|
23 |
04 |
27 |
Jedwali Na.24: SHULE ZENYE KIDATO CHA V-VI |
|||
WILAYA
|
SERIKALI
|
ZISIZO ZA SERIKALI
|
JUMLA
|
Misungwi
|
01 |
- |
01 |
JUMLA:
|
01 |
- |
01 |
Jedwali Na.25: MAHITAJI YA WALIMU, WALIOPO NA UPUNGUFU HADI DESEMBA 2016
WILAYA |
MASOMO YA SANAA |
MASOMO YA SAYANSI |
||||
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
MAHITAJI |
WALIOPO |
UPUNGUFU |
|
Misungwi
|
252
|
442
|
+190
|
220
|
104
|
116
|
JUMLA
|
252
|
442
|
+190
|
220
|
104
|
116
|
Jedwali Na. 26: SAMANI ZA SHULE ZA SEKONDARI, HADI DESEMBA 2016
WILAYA
|
MADAWATI |
MEZA ZA WALIMU |
VITI VYA WALIMU
|
KABATI ZA WALIMU |
||||||||
MISUNGWI
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu/Ziada
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
JUMLA
|
9,164
|
9,274
|
110
|
615
|
252
|
363
|
687
|
311
|
376
|
312
|
70
|
242
|
Jedwali Na.27: IDADI YA MAJENGO KATIKA SHULE ZA SEKONDARI:
|
||||||||||||
WILAYA
|
MAKTABA
|
UTAWALA
|
KUMBI
|
HOSTEL/BWENI
|
||||||||
MAH
|
YAL
|
UP
|
MAH
|
YAL
|
UP
|
MAH
|
YAL
|
UP
|
MAH
|
YAL
|
UP
|
|
Misungwi
|
23
|
0
|
23
|
23
|
19
|
4
|
23
|
01
|
22
|
23
|
01
|
22
|
JUMLA
|
23
|
0
|
23
|
23
|
19
|
4
|
23
|
01
|
22
|
23
|
01
|
22
|
Ongezeko kubwa la wanafunzi ukilinganisha na uwiano wa walimu na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.
Kutokuwa na vitabu maalum/teule vya kiada kutokana na soko huria la vitabu
Upungufu wa walimu hasa walimu wa sayansi na hesabu
Ukosefu wa hostel, husababisha watoto kupanga mitaani na hivyo kusababisha kupata mimba kwa watoto wa kike na kushindwa kumaliza masomo yao
Baadhi ya wanafunzi hutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, hufika wamechelewa na wamechoka na kushindwa kufuatilia masomo
Ukosefu wa nyumba za walimu unasababisha walimu kuishi mbali na shule
Ukosefu wa Library za kutunzia vitabu na kusomea
Utoro wa wanafunzi
Ukosefu wa vitabu vya masomo ya sanaa (Art subjects)
Madeni ya malimbikizo ya mishahara baada ya kupandishwa kwa baadhi ya walimu.
Wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao
Ukosefu wa chakula shuleni husababisha wanafunzi kushinda njaa na kushindwa kufuatilia masomo vizuri
Ukosefu wa vifaa vya maabara hasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Kufanya ufuatiliaji mashuleni na kuhakikisha walimu waliopo wanawasimamia wanafunzi ipasavyo.
Kushiriki vikao vya WDC ili kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo mashuleni, mfano; Utengenezaji wa madarasa na Ukarabati wa miundombinu ya shule.
Kutoa maelekezo kwa watendaji wa Kata kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi na kuwachukulia hatua wazazi wanaoendekeza utoro mashuleni.
Kuendesha vikao kwa wakuu wa shule na waratibu Elimu Kata ili kuwajengea uwezo wa kusimamia shule zao kwa ubora zaidi.
Halmashauri kuwashirikisha wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hostel kwa wanafunzi wa kike.
Wilaya inaendelea kuhamasisha wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuwaandaa kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.
Lengo la afya ya msingi ni kuelekeza huduma za kinga na tiba karibu na wananchi kwa kushirikisha jamii, hadi sasa Wilaya imeweza kupanua huduma toka vituo 41 vya kutolea huduma za afya hadi kufikia vituo 46, ambayo ni sawa na asilimia 39 ukilinganisha na vijiji 113 vilivyopo. Pia kuna ujenzi unaendelea wa Zahanati za Mapilinga, Mwamaguha na Ng’obo na ujenzi huu umefikia hatua ya ukamilishaji na ujenzi wa Zahanati ya Nyang’homango ujenzi upo katika hatua za ukamilishaji.
Halmashauri imeweza kupanua kituo cha afya cha Misasi kwa kujenga chumba cha upasuaji ili kuboresha afya ya uzazi,.pia bado ina mpango wa kupanua vituo vya Afya vya Busongo, Mbarika na Koromije ili viweze kutoa huduma ya upasuaji.
Huduma ya Uzazi na mtoto inatolewa kwenye vituo 46 vya kutolea huduma za Afya.
Akina mama wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya Afya wameongezeka kutoka 72.1% kwa mwaka 2014 hadi 74.3% kwa mwaka 2015/2016.
Kiwango cha chanjo kwa watoto hadi Desemba 2016, kimepanda kufikia 91% (2015/16), matarajio kwa mwaka 2016/17 ni 120%.
UKIMWI bado ni tatizo kubwa katika wilaya ya Misungwi ingawa ukali wake umeendelea kupungua mwaka hadi mwaka, maambukizo kwa kigezo cha waliopima kwa hiari ni yameshuka kutoka asilimia 6.8 hadi 4.2 hii imetokana na uelewa wajamii kuhusu VVU na UKIMWI ,ingawa bado kuna unyanyapaa miongoni mwa Jamii zetu,kwa pamoja tumeweza kufikia vikundi 30 vya watu waishio kwa matumaini,NGO’s tatu (3) na vikundi 12 vinavyotoa msaada kwa watoto yatima walioko shule za msingi na NGO moja (1) inafanya kazi ya kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.
.Mwaka 2016 kulikuwa na watu 10,457 waliojitokeza kwenye upimaji wa hiari na kati ya hao watu 1,105 sawa na asilimia 10.6 ya waliojitokeza walikutwa na maambukizo ya Virus vya UKIMWI (VVU). Wakati huu mpango wa dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI upo, hivyo watumiaji wa dawa hizo wapo. Kwa kipindi cha miaka 11 iliyopita waliojiandikisha kwa ajili ya kupata dawa za kupunguza makali ya VVU/UKIMWI ni watu 10,725 na walio katika matumizi ya dawa ni 4, 446 tu.
Malaria ni ugonjwa ambao bado unaongoza kwa wagonjwa wengi wanaopata huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya. Jumla ya wagonjwa 45,452 walitibiwa kama wateja wa nje na jumla ya wagonjwa 4,112 walilazwa kwa tatizo la malaria kali (severe Maralia)
Katika swala la kupambana na Malaria Idara ya Afya inafanya shughuli zifuatazo;-
Kutoa tiba sahihi kwa wagonjwa wanaopatikana na vimelea vya ugonjwa wa Malaria baada ya kupima kwa kutumia vipimo vya MRDT.
Ugawaji wa vyandarua kwa akina mama wajawazito wanaohudhuria clinic kwa hudhurio la kwanza pamoja na watoto wa umri wa miezi tisa (9) wanaoenda kupata chanjo ya Surua, zoezi hili linafanyika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma.
Utoaji wa Elimu ya Afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa Malaria kwa jamii, kazi hii inafanywa na wahudumu wa Afya ya Jamii waliopata mafunzo ambao wapo kila Kata.
Kuhakikisha kunakua na upatikanaji wa vitenganishi na dawa kwa ajili ya Malaria.
Ugawaji wa vyandarua 19,154 viligawiwa kwenye Jamii kupitia wanafunzi wa darasa la kwanza kwenye shule za msingi zote Wilayani.
Dawa na vifaa tiba hupatikana kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bohari ya dawa Mwanza (MSD) na toka Fedha ya Mfuko wa Afya ya pamoja (Hearth Busket Fund). Dawa ambazo hutolewa na MSD zimepatikana kwa asilimia 87.13 na dawa ambazo tunanunua kupitia Mfuko wa Afya wa pamoja hununuliwa kwa asilimia 100.
Uchakavu wa miundombinu ikiwemo majengo ya OPD na nyumba za watumishi.
Uchakavu na upungufu wa vyombo vya usafiri ususani Ambulance.
Upungufu wa watumishi wa fani mbalimbali kulingana na ikama halisi kama kada za Madaktari, Mionzi, Maabara, Wazoeza viungo, Macho,Pua na Koo
Ufinyu wa bajeti kulingana na gharama halisi za utoaji huduma za afya
Ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo dawa na vifaa tiba toka bohari ya dawa Mwanza (MSD)
Mwamko mdogo wa Jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya wazee 12,360, kati ya hao wanaume ni 5,982 na wanawake 6,378.kundi hili linapewa huduma za matibabu kwa msamaha. Wazee 2,910
( Me 1,358 na Ke 1,552) wametambuliwa katika Kata za Mbarika, Kasololo, Misasi na Usagara na kupatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu. Vituo vyote vya tiba vinatoa huduma kwa wazee bila Malipo. Katika Hospitali ya Wilaya wazee wanatibiwa katika chumba maalumu.
Wilaya ya Misungwi ina jumla ya walemavu 1523 ambapo kati ya hao wanaume ni 731 na wanawake ni 792.Aidha idadi ya walemavu wa ngozi ( albino) katika Wilaya ya Misungwi ni 137 kati ya hao wanaume ni 64 na wanawake 73.Ili kupiga vita mauaji ya albino mambo yafuatayo yamezingatiwa, kuwatambua albino, kufahamu sehemu wanazoishi na kufanya uchaguzi wa uongozi wao kiwilaya. Uchaguzi ulifanyika mwaka 2015 uhamasishaji kwa jamii umefanyika walindwe chini ya usimamizi wa viongozi wa familia na Uongozi wa Serikali ya vijiji na Kata. Katika Wilaya ya Misungwi idadi ya albino waliouwawa ni 3 tangu mwaka 2007 mpaka sasa. Aidha Wilaya yetu ina shule moja ya msingi ya Mitindo yenye kitengo maalum kwa ajili ya walemavu wakiwemo wa ngozi (Albino). Shule hiyo ina walemavu wa ngozi (Albino) wapatao 91 kati yao wavulana ni 39 na wasichana ni 52 kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza.
Wilaya baada ya kuwajengea uwezo wananchi juu ya athari za mauaji ya Albino, hivi sasa wananchi wamekuwa na uelewa mkubwa hivyo mauaji yamepungua kwa kiwango kikubwa.
Mpango wa kutambua na kuelimisha jamii juu ya matunzo ya watoto waishio katika mazingira hatarishi umetekelezwa katika kata 14 kati ya kata 27 na vijiji 54 kati ya vijiji 113. Jumla ya watoto 7,412 wametambuliwa kati yao 3,842 wa kiume na 3,570 wa kike. Baada ya utambuzi huo jumla ya kamati 54 za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ziliundwa. Zoezi hili la utambuzi lilifanywa na shirika la MOCSO.
Mamlaka ya Maji Mjini Misungwi ni kati ya Mamlaka 5 za makao makuu ya Wilaya katika Mkoa wa Mwanza. Mamlaka ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka 1997 ambayo imerekebishwa na Sheria Na. 12 ya mwaka 2002.
Mamlaka ina jumla ya Wateja wapatao 1402 katika makundi ya fuatayo:
Maji manyumbani - 1308.
Maji Biashara - 38
Maji Taasisi - 44
Magati ya kuchotea Maji - 12
Mji wa Misungwi una jumla ya watu/wakazi wapatao 41,224, idadi hii inajumlisha vitongoji vya Mwambola, Mapilinga, Nange, Mwajombo, Iteja na Misungwi yenyewe. Mahitaji ya maji yanakisiwa kuwa meta za ujazo 3273 kwa siku, wakati uzalishaji toka chanzo cha Nyahiti (Ziwa Victoria) ni meta za ujazo 600 kwa siku (600m3/Day) sawa na asilimia 18 ya mahitaji ya Jumla ya watu wapatao 21,000 wanaopata huduma ya maji.
Kuna jumla ya miradi miwili ambayo ni Nyahiti intake (Chanzo ni Ziwa Victoria) na Mitindo dam (Bwawa la Mitindo) na yote yanafanya kazi.
Ni mradi uliokuwa ukihudumia wakazi wa mji wa Misungwi, baada ya mradi toka ziwa Victoria kukamilika ulibaki kuwa wa dharura. Mradi wa mitindo una mabwawa madogo matatu ya kuhifadhi maji(Three Storage Tanks) yenye ujazo tofauti yaani 50m3,30m3 na 12m3 na yana uwezo wa kuhifadhi jumla ya Meta za ujazo tisini na Mbili (92m3).
Upatikanaji wa maji haulingani na mahitaji ya wakazi wa Mji wa Misungwi kwa sababu zifuatazo:-
Yote haya yanatarajia kutekelezwa kupitia mradi mkubwa wa kuboresha miundo mbinu ya maji kwa miji ya Misungwi, Magu, Lamad, Bukoba, Musoma na Mwanza na, unaofadhiliwa na Benki ya uwekezaji ya Ulaya (EUroppean Investment Bank) (EIB) na Shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD - Agency for French Development).
Lengo kuu la sekta ya maji ni kuhakikisha kwamba wananchi wa Misungwi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa gharama nafuu mita 400 kutoka kwenye chanzo hadi kwenye kaya .Idadi ya watu wanaopata huduma yamaji safi na salama vijijini na mjini ni 150,565 ambayo ni sawa na asilimia 43 ya jumla ya watu 351,607 waliopo wilayani.
Katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 Halmashauri kupitia Idara ya Maji imepanga kukamilisha ujenzi wa miradi mitatu ya Maji bomba katika vijiji vya Igenge,Ngaya- Matale,Matale –Manawa – Misasi kupitia Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri COWI Tanzania na usimamizi wa ndani kupitia Halmashauri na Secretarieti ya Mkoa.
a) Ujenzi wa Mradi wa Maji bomba Igenge
Mradi huu unajengwa na Mkandarasi aitwaye Seekevim Ltd wa Dar-es salaamu. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni:
Mradi huu unajengwa na mkandarasi aitwaye CMG Construction Co.Ltd wa jijini mwanza. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni:-
Mradi huu unajengwa na mkandarasi aitwaye Syscon Builders Construction Ltd wa Dar-es-salaam. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa kwa mujibu wa mkataba ni:-
Jedwali Na.28.: Wastani wa Utoaji wa Huduma ya Maji safi Wilayani |
||||
Wilaya |
Idadi ya Vijiji |
Idadi ya watu |
Idadi ya watu wanaopatiwa huduma ya maji |
Kiwango cha asilimia |
Misungwi
|
113
|
351,607
|
150,565
|
43
|
Hali ya utumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ni kama ilivyo katika Halmashauri zingine, tunakumbwa na uhaba mkubwa katika kada za Afya, Elimu na Kilimo. Kwa ujumla Halmashauri ina watumishi wapatao 3,011 kati ya mahitaji halisi ya 4,214 hivyo kufanya upungufu wa watumishi kufikia1,203. Aidha tunaendelea na mpango wa kuhakikisha kuwa nyumba za watumishi zinajengwa ili kuhakikisha kuwa watumishi hao wanapata mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Hadi sasa Halmashauri imeshajenga nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri. Bado tunaomba Serikali kuendelea kutusaidia kujenga nyumba zingine zaidi ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumishi.
Serikali kwa kupitia Vyombo/Taasisi mbalimbali, imefanikiwa kufanya Uhakiki wa watumishi kwa kuangalia Taaluma zao, aidha watumishi wachache wameweza kubainika kujipatia ajira kwa udanganifu na wengine kutowajibika ipasavyo. Hali hii imepelekea Mamlaka za kinidhamu kuwafukuza na wengine kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu.
Wilaya ya Misungwi inazo Benki mbili za NMB na CRDB zinayotoa huduma kwa wananchi wake. Pia kuna SACCOS ya MKUKUWAMI ambayo hutoa mikopo kwa wanachama wake na Taasisi za kifedha kama Maboto ,Bayport,Equity,Faidika
Wilaya ya Misungwi imebahatika kuwa na mitandao ya simu kutoka katika makampuni ya simu mbalimbali na kuwafanya wananchi wake kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa zao katika kuboresha mahusiano ya kijamii na kibiashara. Makampuni ya simu yanayotoa huduma za simu ni kama ifuatavyo; Kampuni za Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL, Halotel na Zantel. Aidha bado kuna changamoto katika maeneo mengi ya vijijini ambako makampuni hayo bado hayajaweka minara yao ili kuongeza mtandao wa huduma hizo.
Wilaya inatoa shukrani kwa Serikali yetu kwa kuiwezesha Jamii kupata miradi ya maendeleo ambayo itatoa matokeo ya muda mfupi na haraka “Big Results Now –BRN” na imechangia kuboresha miundo mbinu mjini na vijijini, ambayo itaboresha hali ya maisha kwa kuongeza vipato kwa walengwa.
Naomba kuwasilisha
JUMA S. SWEDA
MKUU WA WILAYA
MISUNGWI
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.