Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw. Abdi Makange amewataka Madiwani kuitunza thamani waliopewa na Wananchi katika utatuzi makini wa changamoto zao na kuwapekeka Maendeleo.

Amesema hayo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kilichofanyika 03/12/2025 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kilichojadiliwa Uapisho wa waheshimiwa Madiwani, Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, kuunda kamati za kudumu za Halmashauri, kupokea taarifa mbalimbali za shuguli za Halmashauri kwa Kipindi cha Julai hadi Novemba na kupitisha Ratiba ya vikao vya Halmashauri.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe. Ibrahim Masalu Kaswamwa amewashukuru na kuwapongeza Waheshimiwa madiwa na kutoa rai kuendelea kushirikiana na Baraza hilo kwa kuhakikisha maendeleo na Changamoto za Wananchi zinafuatiliwa kwa ajili ya kuzitatua.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe. Ibrahim Masalu Kaswamwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amesema kuwa wataendeleza ushirikiano na bidii katika kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inaendelea kufanikishwa kwa kushirikiana na wakuu wa idara,vitengo,wakuu wa Taasisi na watendaji ngazi ya kata na vijiji.

Mkurugenzi Mtendaji H/W Misungwi Bw. Addo Missama
Pia Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Silvery Luboja Salvatory amewapongeza Madiwani wote waliochaguliwa na kuwasihi kuwa muda huu ni wa kufanya kazi kwa yale tulionadi kwa wananchi vilevile taarifa ya Halmashauri imepokelewa na kuhakikisha inafanyiwa kazi. amewapongeza Madiwani wote waliochaguliwa na kuwasihi kuwa muda huu ni wa kufanya kazi kwa yale tulionadi kwa wananchi vilevile taarifa ya Halmashauri imepokelewa na kuhakikisha inafanyiwa kazi.

Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Silvery Luboja Salvatory
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.