HUDUMA NA SHUGHULI ZINAZOTOLEWA NA IDARAYA MAJI VIJIJINI NA MJINI
Idara ya maji kwa ujumla inashughulika na utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi waishio mjini na vijijini kupitia vyanzo mbali mbali vya maji.
Idara ya Maji ina vitengo viwili(2) ambavyo ni Maji Mjini na Vijijini. Huduma ya maji Mjini kwa sasa inatolewa kwa kiawango cha asilimia 42 kwa watu waishio mjini ,wakati Vijijini huduma ya maji ya inatolewa kwa asilimia 43. Kiwilaya Watu wanaopata huduma ya maji safi na salama ni asilimia 43 kati ya wakazi wote wa Wilaya ya Misungwi wapatao 351,607.
Vyanzo vinavyotumika kutoa huduma hii ni :-
NA
|
AINA YA CHANZO
|
IDADI
|
VINAVYOFANYA KAZI
|
VISIVYOFANYA KAZI
|
1
|
Visima virefu
|
6 |
5 |
1 |
2
|
Visima vifupi
|
352 |
216 |
136 |
3
|
Miradi ya usambazaji
|
14 |
9 |
6 |
4
|
Matenki ya kuvuna maji ya mvua
|
55 |
40 |
15 |
5
|
Mabwawa
|
4 |
3 |
1 |
6
|
Miradi ya usambazaji (KASHWASA)
|
5 |
5 |
0 |
Miradi yote tajwa hapo juu inaendeshwa na vyombo vya watumiaji maji (COWSOs), Taasisi za Umma na Binafsi na kamati za maji za vijiji (VWC) au Vikundi vya watumiaji maji (WUGs) kama ivyosisitiza Sera ya Maji ya mwaka 2002 na Sheria ya maji ya mwaka 2009 Na.12
Hadi sasa Halmashauri imeshaunda na kusajili vyombo vya Watumiaji Maji (COWSOs) 27 katika vijiji mbalimbali vya Halmashauri na COWSO 1 siyo hai.
2.0 MAJUKUMU YA IDARA YA MAJI VIJIJINI NA MJINI
Kuandaa na Kuwasilisha bajeti ya Sekta ya Maji katika Halmashauri
Kuandaa usanifu wa miradi ya maji pamoja na kusimamia ujenzi wake kwa kuzingatia maombi kutoka vijijini
Kusimamia ujenzi wa miradi inayotekelezwa na wakandarasi.
Kusimamia kazi za Wataalam Washauri na wakandarasi walioajiriwa na Halmashauri wanaotekeleza kazi za maji.
Kusaidia sekta binafsi kutayarisha makubaliano au mapatano baina ya wilaya na vijiji, na kati ya vijiji na wakandarasi
Kufuatilia shughuli za sekta binafsi wanaofanya shughuli za maji na kutoa ushauri.
Kusaidia vijiji kuunda vyombo vya uendeshaji wa miradi ya maji
Kutayarisha miongozo ya uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji itakayosaidia vijiji.
Kupanga na kuratibu mzunguko wa maendeleo ya miradi ya maji (project cicles) kwa wananchi katika sekta za umma na za watu binafsi kuhusu usambazaji maji wilayani.
Kuainisha mpango wa maendeleo ya miradi ya maji na bajeti ya mwaka ya Halmashauri ya wilaya na mpango wa maendeleo ya sekta ya maji wa Taifa.
xi) Kutathmini miradi ya maji vijijini kutokana na maombi ya vijiji.
xii) Kutoa utaalam kuhusu upimaji na usanifu wa miradi ya maji kwa wadau wanaohusika na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani.
xiii) Kuainisha usanifu wa ujenzi wa mradi na usanifu wa tekenolojia ya uendeshaji na matengenezo ya miradi wakati wa utayarishaji wa mipango ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi.
Kufuatilia na kuhakiki usanifu unaofanywa na wahandisi washauri binafsi waliongia mkataba na Halmashauri au vijiji kwa kazi husika.
Kushauri vijiji kuhusu jinsi ya kushiriki kikamilifu katika kuchagua na kutayarisha miradi ya maji
Kusaidia utayarishaji wa mapatano na makubaliano baina ya wilaya na vijiji, au vijiji na wakandarasi, kwenye kutekeleza miradi ya maji mahali ambapo wakandarasi wanatumika.
Kuratibu na kutoa ushauri unaohitajika kwenye jumuiya ya vijiji kwenye utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji
Kukusanya takwimu mbalimbali kutoka vijijini na kuzifanyia kazi ili zifikie hatua ya kuwa taarifa zinazoweza kufanyiwa kazi.
Kuweka takwimu zote za miradi ya maji za Halmashauri na sekta binafsi (benki ya takwimu) ili kusaidia katika kupanga miradi mbalimbali wilayani.
Kuhamasisha maendeleo ya wananchi kwa kuhifadhi na kutumia rasilimali ya maji.
Kuhifadhi taarifa kwenye kompyuta na kuzisambaza taarifa hizo zinakohitajika.(ndani na nje ya ofisi ya Mhandisi wa Maji wa Wilaya).
Kufanyia uchambuzi na kutathmini mfumo wa utunzaji habari na kuboresha mfumo wa kutunza kumbukumbu hizo.
Kuandaa taarifa za kila mwezi kuhusu shuguli za sehemu ndogo.
Kuratibu na kusimamia utunzaji wa mazingira wa vyanzo vya maji
Kuchukua hatua zinazostahili baada ya ukaguzi kufanyika kwa lengo la kuepusha na kurekebisha endapo uharibifu umejitokeza.
Kushiriki katika kutoa elimu ya afya na usafi wa mazingira kwa jamii wakati wa ujenzi wa miradi ya maji.
Kuelimisha jamii kuhusu uondoshaji wa maji yaliyotumika, matumizi bora ya maji na ujenzi wa vyoo bora.
Kukagua, kushauri na kusaidia jamii katika utunzaji wa mazingira.
Kuhakikisha usafi wa mazingira katika vyanzo vya maji ili kulinda afya za watumiaji maji.
Kuratibu na kutathmini uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji pamoja na kutoa utaalam kwenye vijiji kuhusu uendeshaji na matengenezo ya miradi.
Kuhakiki usanifu na uwekaji wa tekenolojia ya uendeshaji na matengenezo ya miradi inayojengwa na wakandarasi au na sekta binafsi.
Kutayarisha miongozo ya uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji ambayo itaendeshwa na vijiji au sekta binafsi.
Kufuatilia uendeshaji na matengenezo ya miradi inayoendeshwa na watu binafsi au vijiji.
Kutoa utaalam kwenye ngazi ya vijiji katika kushirikisha taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa pamoja na za watu binafsi kwenye uendeshaji na matengenezo ya miumdombinu ya miradi ya maji.
Kusaidia na kutoa utaalam kwenye vijiji katika kununua mashine na pampu za kusukuma maji, zinazostahili
Kushirikiana na Timu ya Wilaya ya wataalam inayoshughulika na masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira katika kutayarisha zabuni mbalimbali zitakazotumiwa na Halmashauri na sekta binafsi katika uendeshaji wa miradi ya maji
Kutoa ushauri wa kitaalam kwa vijiji katika kuandaa vyombo vyao vya uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji
Kukagua, kutathimini na kuratibu ubora wa maji kabla na baada ya ujenzi wa miradi na wakati wa uendeshaji.
Kupitia miongozo na mifumo ya ujazaji wa takwimu ya uendeshaji na matengenezo kutoka Wizarani na kuisambaza vijijini na inapo bidi kuitolea maoni.
Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kitaaluma kuendesha miradi yao.
Kutoa mafunzo mbalimbali kwa wananchi juu ya menejimenti ya mifumo ya ujazaji wa uendeshaji wa miradi yao.
3.0 WATUMISHI
Kwa sasa Idara ya Maji ina Watumishi 17 kwa mchanganuo ufuatao hapa chini:-
i) Mkuu wa Idara Mhandisi wa Maji wa Wilaya
ii) Wahandisi - 1
iii) Mafundi Mchundo - 2
iv) Mafundi Mchundo Wasaidizi -5
v) Wasaidizi wa Ofisi – 8
Kutokana na muundo wa Idara,kuna upungugufu wa watumishi 18 wenye sifa mbalimbali
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.