Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amewapongeza Viongozi wa Waafisa Usafirishaji Kanda ya Misungwi Kwa namna Walivyoandaa Bonanza la Maafisa Usafirishaji Wakati akifunga Mashindano ya Maafisa usafirishaji.

Ametoa pongezi hizo Leo Tarehe 27 Oktoba 2025 ambapo amwasisitiza pia Kujitokeza kwa wingi Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tarehe 29/10/2025 kupiga kura na kurudi nyumbani kwa Amani na Utulivu.

Naye Katibu.wa bodaboda kanda ya misungwi Mjini Bw.Yohana Simoni Kiyuga ameshukuru sana ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwaunga mkono pamoja na ushirikiano toka kuanza kwa bonanza mpaka mwisho

Bonanza hilo limeshuhudia michezo Mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu ,Kukimbiza Kuku,kuimba na kucheza Mziki.

Aidha Mshindi wa Mpira wa Miguu ni Maafisa Usafirishaji Kona ya Mitindo wameibuka na ushindi wa Magori Mawili kwa Moja dhidi ya Maafisa Usafirishaji wa Stend kwa Magori ya Emmanuel dakika ya 22 na Msonda Elisha Dakika 38 na Gori la Kufutia machozi la la Maafisa Usafirishaji stand limefungwa na Lazaro Kamala dakika ya 50 pia Katika Mashindano hayo Mchezaji bora ni Zabroni Doha

kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu 2025 "kura yako, Haki yako jitokeze kupiga kura"
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.