Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe,Suleiman Jafo ameiagiza Menejimenti ya Halmashauri ya Misungwi kuweka Mpango wa Bajeti ya Fedha kwa mwaka 2018/2019 kwa ajili ya Ujenzi na kuboresha miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ili kuongeza na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya kwa Wananchi Wilayani humu.
Mhe,Jaffo ametoa agizo hilo wakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya Wilayani humu kwa lengo la kuongea na Watumishi pamoja na kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwaWilayani Misungwi ambapo ameweza kutembelea katika Hospitali ya Wilaya na katika Shule ya Sekondari ya Misasi na kuona hali halisi ya miundombinu iliyopo katika maeneo hayo.
Pichani Juu ni Mhe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akikagua Miundombinu katika Jengo la Maabara iliyokamilika katika Shule ya Sekondari Misasi.
Mhe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Selemani Jafo akisikiliza maelezo na ufafanuzi wa mikakati ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Sekta ya Elimu kutoka kwa Afisa Elimu Wilaya ya Misungwi,Bi,Dianah Kuboja (Kulia )wakati alipotembelea katika Shule ya Sekondari Misasi.
Waziri Jafo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuandaa Mikakati na kuweka mpango katika Bajeti ya mwaka 2018/2019 ya kujenga na kuboresha miundombinu ya Hospitali ikiwemo Ujenzi wa Jengo la Upasuaji,ujenzi wa Wodi ya akina Mama pamoja na Jengo la kuhifadhia Maiti(Mortuary)aliagiza haya mara baada ya kutembelea katika Hospitali hiyo ambapo akabaini baadhi ya changamoto za kutokuwa na majengo yanayokidhi matakwa ya utoaji wa huduma za afya katika ubora na uhakika na yanayovutia katika utendaji kazi wa Wataalam wa Afya.
Waziri wa Nchi Ofis ya Rais,TAMISEMI Mhe,Selemani Jafo akimuuliza maswali Mganga Mfawidhi wa Hospitali Bi. Macelina Kiemi kuhusu utoaji wa huduma ya malipo kwa Wagonjwa kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki katika Dirisha la Mapokezi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ambapo kwa Takwimu zinaonyesha kwamba makusanyo kwa mwezi yanafikia Tsh,Milioni 4.
Waziri Jafo alipongeza juhudi za Halmashauri hiyo kupitia kwa Afisa Elimu wa Sekondari kwa kuinua kiwango na ubora wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Misasi ambayo imepata ufaulu wa daraja la kwanza Wanafunzi 7 na kupeleka Wanafunzi 40 kidato cha Tano kati ya Wanafunzi 100 waliofaulu Shuleni hapo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.