Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe,Profesa Makame Mbarawa aagiza Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nyahiti Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza kukamilisha kazi ya ujenzi wa Mradi huo mwezi Machi mwaka 2019 ili kuondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa Misungwi
Waziri Mbarawa, amemtaka Mkandarasi huyo wa Kampuni ya CCECC ya China inayojenga Mradi huo, kukamilisha ujenzi mwezi Machi mwaka 2019, wakati wa Ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli na maendeleo ya ujenzi huo Wilayani Misungwi na kuitaka Mamlaka ya Maji Safi Mwanza MWAUWASA kufuatilia na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa kiwango na kwa wakati mapema mwezi Machi mwaka 2019 badala ya mwezi Mei kwa mujibu wa Mkataba na kuzingatia makubaliano ya Mkataba.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe,Profesa Makame Mbarawa akizungumza na kuagana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Antony Bahebe Masele akiwa pamoja Madiwani wengine Wajumbe wa Kamati aya Fedha,Uongozi na Mipango.
Mhe,Mbarawa alisema kwamba Mradi huo utagharimu shilling Billioni 9.3 ambazo ni fedha za mkopo wa masharti nafuu na utakuwa unatoa maji safi na salama takribani lita millioni 4 na nusu kwa siku na kueleza kuwa Wananchi wa Misungwi waliokuwa wanapata maji safi na salama walikuwa ni asilimia 43 tu hivyo kulikuwa nachangamoto kubwa ya ukosefu wa maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe, Profesa Makame Mbarawa akishiriki kuchimba Mtaro wa Bomba la mfumo wa Maji safi na Salama katika Mradi wa Maji wa Nyahiti Wilayani Misungwi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Juma Sweda ameishukuru Serikali kwa kupanga na kutoa fedha za kutekeleza mradi huo wa maji ambao utahudumia Wananchi wa Mji wa Misungwi na maeneo jirani na kusababisha kufikia kiwango cha upatikanaji wa maji kufikia asilimia 75 kwa Wananchi wote.
Mkuu wa Wilaya huyo ameeleza kwamba wataendelea kufuatilia kwa karibu na kutoa ushauri wa mara kwa mara kwa wasimamizi wa mradi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba baina ya Mkandarasi na Serikali ili kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kulingana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 -2020.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.