Serikali yaridhishwa na utekelezaji wa shughuli za mpango wa kunusuru kaya maskini uliogharimu shilingi Bilioni 19.4 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Hayo yamebainishwa Agosti,04,2023 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe, Boniphace George Simbachawene wakati akikagagua Mradi wa Mpango wa kunusuru Kaya maskini ambapo amesema kuwa Serikali imetekeleza Mradi wa kupunguza umaskini kwa kuanzisha miradi ya ujenzi wa barabara za jamii,uchimbaji wa malambo,visima vifupi na upandaji miti.
Waziri Simbachawene amesema kwamba katika kukuza kipato na kuboresha uchumi wa kaya Serikali imetoa ajira za muda,miradi ya miundombinu na miradi ya shughuli za kuongeza kipato cha kaya,ambapo kupitia miradi hiyo wananchi wamenufaika kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kuchumi kama biashara ndogondogo,kilimo,ufugaji,ushonaji na kuboresha makazi yao na kaya kujiunga na mfuko afya ulioboreshwa.
Wakati wa ziara yake Mhe, Simbachawene alitembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekonadari ya Wasichana Mwanangwa iliopo Kata ya Mabuki inayojengwa kwa fedha za Serikali kupitia mpango wa Tasaf ambao umegharimu zaidi Milioni 160 na kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi huo na thamani ya fedha imeonekana,na kuagiza kujengwa kwa uzio,kutengeneza viwanja vya michezo,kupanda miti na maua ili kuvutia wanafunzi katika kujifunza.
Wakati huo huo Mhe, Waziri Siibachawene awali alizungumza na Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika ukumbi wa Halmashauri na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni taratibu na sheria ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku ambapo amewataka Viongozi kuwatendea haki na mema wananchi na watumishi ili kuleta furaha na Amani miongoni mwao.
“Viongozi wanapaswa kufanya kazi kama wazazi kwa kutoa usahauri na kuelekeza vizuri namna ya kutatua changamoto walizonazo watumishi kwa lengo la kuleta maendeleo na kujenga Taifa”.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti ameipongeza na kushukuru Serikiali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi ya Miradi mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya,Elimu pamoja na Maji ambapo amsema Serikali tayari imetoa fedha ya kutosha katika Mradi wa Maji kutoka Mbarika hadi Mabuki ambapo mradi utakapokamilika wananchi wa Misungwi watanufaika kupitia mradi huo kwa kupata maji safi na salama.
Mnyeti amesema Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Mwangwa ,Misasi hadi Kahama utajengwa kwa kiwango cha lami na tayari fedha imeshatengwa kwa ajili ya mradi huo ambapo itakapokamilika itarahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja usafiri kwa wananchi wa Misungwi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Paulo Chacha amesema Serikali haitafumbia macho kamwe kwa mtu yeyote ambaye atathubutu kuwarubuni Wanafunzi kwa namna yeyote ile au watu wenye nia mbaya ya kutaka kukwamisha ndoto za wanafunzi ili kutofanikisha ndoto zao na malengo yao ya baadaye waliojiwekea.
“Pamoja na kuwahakikishia watoto hawa kama unavyowaona wanapendeza kufikia ndoto zao kama walivyokusudia bila kupepesa jicho wala kurudi nyuma kila mmoja na shughuli yake lazima itimie kwa mujibu wa taratibu zilizopo na lazima wayafikie malengo yao kama walivyojipangia”.
Mhe, Diwani wa Kata ya Mabuki Bw,Petro Malale akitoa shukrani zake za pekee mbele ya wakazi wa Mabuki kwa Serikali kwa kuleta fedha kwa ajili ya kukamilisha Miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa inayojengwa kwa fedha za Serikali kupitia Mpango wa Tasaf
Wananchi wa Kijiji cha Mwanangwa kata ya Mabuki kwa ujumla wake wakiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Boniphace George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekonadari ya Wasichana mwanangwa hapo jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Boniphace George Simbachawene akihutubia wakazi wa kijiji cha Mwanagwa jana wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa ujenzi waShule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa,ambapo aliridhishwa na hatua ya ujenzi huo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.