Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Kassimu Majaliwa Majaliwa aridhishwa na kasi ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Misungwi mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi huo mapema jana katika eneo la Fela Waziri Mkuu ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo uliofikia asilimia 14 ya ujenzi kwa sasa.
Amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi na kujituma pamoja na kuhakikisha kwamba wanautumia ujuzi na maarifa ya ufundi wanaopewa na watalaalam wa kutoka nje ya Nchi na kuendeleza kazi za ujenzi na ukarabati mara baada ya kukamilika kwa mradi huo..
Waziri Mkuu Majaliwa amekemea vitendo vya baadhi ya Wananchi wenye tabia ya kudokoa na kuiba vifaa vya ujenzi wa reli ya kisasa SGR ambapo amelitaka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kuwachukulia hatua Wananchi watakaobainika kufanya uhalifu na wizi wa mali za mradi huo, na kuwaomba Wananchi kuendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na kulinda mali za mradi ili zitumike kwa ajili ya faida ya Watanzania wote.
Naibu Waziri wa Ujenzi ,Godfrey Kasekenya amesema kwamba ujenzi wa Reli ya kisasa kwa kipande cha Mwanza hadi Isaka wenye kilomita 341ambao unajengwa kwa shilingi Trioni 3.4 unaendela vizuri na Mkandarasi kutoka Nchini China anfanya kazi kwa weledi na Serikali inaendelea kusimamia mradi huo kwa karibu na kuhakikisha malipo yanatolewa kwa wakati.
Mhandisi Kasekenya amebainisha baadhi ya faida na manufaa yatakayopatikana mara baada ya ujenzi wa reli kukamilika ni pamoja na kurahisisha Usafirishaji wa Abiria na mali na usafirishaji wa mizigo ya kibiashara ikiwemo bidhaa za Viwandani na mazao kwa ajili ya biashara na Chakula kwa Wananchi na kuwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wafanyakazi wa mradi ili kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa haraka na kwa ufanisi Zaidi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo nla Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti ameipongeza na kushukuru Serikiali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi ya miradi ya Maji takribani Bilioni 10 pamoja na miradi ya sekta ya Elimu, Afya na miundombinu na kwamba Viongozi wa Wilaya wataendelea kuisimamia kikamilifu Miradi na kukamilika kwa ubora na viwango ili iwanufaishe Wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Rasilimali wa Shirika la reli nchini Bi. Amina Lumuli amesema ujenzi wa mradi huo umefikia hatua ya asililimia 14 na kueleza kwamba kupitia mradi wa ujenzi wa Reli wameweza kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya wafanyakazi 5400 katika kazi tofauti tofauti pamoja na ufundi na Shirika la reli linaendelea kusimamia kikamilifu ujenzi huo.
Wakati huo huo Mhe, Majaliwa awali alikagua Ujenzi wa Mradi wa kimkakati wa Daraja la JPM la Kigongo hadi Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 na tayari limefikia asilimia 53 za ujenzi ambapo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha Bilioni 699 na ameridhika na hatua za ujenzi na kueleza kwamba Serikali inaendelea kutoa fedha za malipo ya mradi huo kila baada ya hatua moja ya ujenzi kukamilika na kuhakikisha kwamba fedha za mradi zipo.
Amesema kwamba hatua hiyo iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo ni ya kujivunia kwa sababu mradi huo utakapokamilika utawezesha Wananchi kusafiri na kusafirisha mizigo yao kwa urahisi na kuongeza kipato na uchumi wa taifa.
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti kushoto, kulia ni Waziri Mkuu Mhe, Kassimu Majaliwa akiongea na wananchi waliofika katika ziara ya Mhe,Waziri Mkuu hapo jana eneo la Fela ambapo ameishukuru Serikali kwa kuleta Fedha za Miradi zaidi ya shilingi Bilioni 10 za Miradi ya Maendeleo ikiwa pamoja na maji.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Fela wasikiliza kwa makini Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa ziara yake hapo jana alipokuwa akikagua Mradi wa Reli ya kisasa ya Mwanza hadi Isaka ambapo amesema Mradi huo umegharimu Trioni 3.4
Mwonekano wa picha ya kipande cha Reli ya kisasa(SGR) ya Mwanza hadi Isaka ambapo itakapokamilika itarahisisha usafiri wa abiria pamoja na mizigo .
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.