Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa aridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa daraja la John Pombe Magufuli lnaloendelea kujengwa katika eneo la Kigongo hadi Busisi Mkoani Mwanza.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwamba amefurahishwa na kazi inayofanywa na Mkandarasi wa Kampuni ya Nchini ambayo inafanya kazi chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri Abdulkarim Majuto anayehakikisha masuala yote ya uhandisi na taratibu za ujenzi wa madaraja zinafuatwa na kuzingatiwa.
Waziri Mkuu Majaliwa ametembelea na kuona kazi ya ujenzi wa mradi huo mapema Desemba 18 mwaka 2020 na kupatiwa maelezo ya namna ujenzi unavyofanyika kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Daraja, Abdulkarim Majuto, aliyetoa maelezo ya kina ya ujenzi huo ambao unagharimu takribani shilingi Bilioni 699.2 kwa kujenga daraja lenye urefu wa kilomita 3.2 na yenye barabara unganishi yenye kilomita 1.66 ambapo ujenzi unaendelea vizuri.
Amesema kwamba Serikali inaweka na kujenga miradi mikubwa ya maendeleo ikiwa ni kukabiliana pia na changamoto ya ajira na kuwapatia Wananchi fursa za ajira ambapo wanaweza kujipatia fedha za kuendesha maisha yao ya kila siku, na kwa taarifa zilizopo katika mradi huu mkubwa unaajiri zaidi ya Watanzania 370 ambao wanafanya kazi mbalimbali katika mradi huu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti amemshukuru Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutenga fedha tena za mapato ya ndani na kodi ya Watanzania kwa ajili ya ujenzi wa daraja hili la ajabu ambalo litaokoa na kusaidia maisha ya Wananchi katika usafirishaji wa abiria na mizigo yao.
Amewataka Wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo na kumhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kwamba Wananchi wa Misungwi wataendelea kufanya kazi na kuchapa kazi ipasavyo na kuongeza mapato na uchumi wa taifa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea maelezo na kuhoji na namna taratibu za ujenzi wa Daraja la JPM, na hatua zinavyoendelea na kuhakikisha ujenzi unafanyika katika ubora na viwango vya madaraja hapa Duniani.
Mwonekano wa ujenzi wa Daraja la JPMunavyoendelea kwa kasi kwa upande wa kushoto ni daraja la muda kwa ajili ya kupita ili kusaidia mitambo na vifaa vya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 699.2
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.