Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa awataka Watendaji wa Serikali kufuatilia shughuli za Miradi ya Maendeleo Vijijini ili kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo wakati anazungumza na Watumishi wa Serikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mitindo akiwa katika Ziara ya Kikazi kwa ajili ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Waziri Mkuu Mhe,Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri .
Mhe,Majaliwa pia alifungua Mabweni ya Wanafunzi katika Shule ya Msingi Mitindo lenye gharama ya shillingi 150,000,000 litakalobeba Wanafunzi 84,kukagua Shamba la Pamba la Hekari 6 lililolimwa na Mhoja Ngole wa Kijiji cha Mondo,kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Mbarika -Manawa utakaohudumia Vijiji 12,pamoja na kuweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Gulumungu iliyojengwa kwa nguvu za Wananchi na fedha za Serikali,na tayari vyumba vinne vya Madarasa,Ujenzi wa Nyumba 1 ya Mwalimu ,na Ujenzi wa Jengo la Utawala kwa gharama ya shillingi 74,523,216.62.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.