Watu wenye Ulemavu watakiwa kutumia fursa za Mikopo kubadili maisha yao Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Diwani wa Kata ya Usagara Mhe,Kashinje Machibya amewataka Watu wenye Ulemavu kutumia fursa za Mikopo ya asilimia 10 asilimia ambapo asilimia 2 ni ya Watu wenye ulemavu wakati wa Maazimisho ya siku ya watu wenye Ulemavu.
Hayo yamesemwa tarehe 3/12/2022 kwenye maazimisho ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Maalumu ya Mitindo Misungwi ambapo amewataka Watu wenye ulemavu kukopa na kurejesha mikopo hiyo isiyokuwa na riba ili kuweza kujikwamua kwa kufanya shughuli za maendeleo na kujipatia kipato ambapo mikopo hiyo inatolewa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Bwana Machibya amesema kuwa Mwaka wa fedha 2022/2023 wametenga zaidi shilingi Bilioni moja ambazo asilimia 40 kwa maendeleo na fedha hizo asilimia 10 ni kwa ajili ya mikopo kwa vikundi.Amesisitiza Ofisi ya Maendeleo ya Jamii waendelee kutoa mikopo kwa uaminifu na uadilifu kwa vikundi mbalimbali kwani fedha ipo kwa ajili yao.
Kwa upande wake Mtaalamu Kiongozi Ujumuishi kwa Wenye Ulemavu Mwl.Benjamin L Kihwele wa Shirika la Sense International Tanzania linalofanya kazi kwa Ushirika na ADD International na Tanzania Cheshire Foundation katika kutekeleza mradi wa Elimu jumuishi uitwao Task Order –T051 kwa Ufadhili wa FCDO kupitia Serikali ya Uingereza amesema kuwa kazi kubwa ya Mashirika haya ni kubaini watoto wenye ulemavu ,kuwapima ESRAC kwa kubaini mahitaji maalumu ya ujifunzaji na kuwaandikisha shule jumuishi jirani na nyumbani kwao.
Vilevile Mwl.Kihwele ameongeza kuwa wamekuwa wakifundisha walimu jinsi ya kutumia mbinu shirikishi za ujifunzaji katika madarasa jumuishi ili kuweza kubaini watoto wenye ulemavu katika mazingira tofauti yanayowazunguka,na kutoa rai wa wadau na wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa kuwatoa watoto wao wenye ulemavu ili wapate huduma bora,Elimu kulingana na kiwango chao; na kuwashukuru Wageni walikwa na wadau mbalimbali waliojitokeza katika Maazimisho hayo.
Kwa upande wake Bw.Malimi Luhanya ambaye ni Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali APDM Mkoa wa Mwanza linalojihusisha na Watu wenye ulemavu amesema kuwa kuna umuhimu wa elimu na mafunzo kutolewa kwa watu wenye ulemavu juu ya mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Halmashauri isiyo kuwa na riba ambapo asilimia 2 ni kwa watu wenye ulemavu ili wawe sifa na vigezo vya kukopesheka na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.Pia Shirika hilo wanatoa ushauri na elimu kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuwajengea uwezo na kuwaandikisha watoto hao kulingana kiwango chao.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bi.Juliana Mwongerezi amesema mikopo ya asilimia 10 inatolewa katika Halmashauri zote nchini bila riba na asilimia 2 ni kwa watu wenye ulemavu ambapo amewaomba kuchangamkia fursa ya mikopo kwa lengo la kuzalisha faida endelevu ili kuweza kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na kuwa mpango mkakati wa kujikwamua sehemu moja kwenda nyingine,na ni ruksa kwa kikundi au mtu mmoja mmoja kukopa kwa watu wenye ulemavu. Bi.Mwongerezi amesisitiza kuwa moja ya vigezo vya Mikopo ni pamoja na uaminifu kwa mwanakikundi katika kukopa.
“Suluhisho la mabadiliko kwa maendeleo jumuishi kwa mchango wa ubunifu katika kuchagiza dunia na yenye Usawa” kauli mbiu.
Mtaalamu Kiongozi Jumuishi kwa wenye ulemavu Mwl.Benjamini Kihwele akiongoza mjadala katika siku ya Maazimisho ya siku ya watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mitindo siku ya Jumamosi tarehe 3/12/2022
Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Kashinje Machibya aliyesimama, akiwa mgeni rasmi katika Maazimisho ya siku ya Watu wenye Ulemavu katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mitindo Misungwi yalifanyika siku ya Jumamosi tarehe 3/12/2022
Baadhi ya viongozi (alivaa suti ya daki bluu katikati ni Mratibu wa APDM Mkoa wa Mwanza)na wadau mbalimbali waliofika katika maazimisho ya siku ya Welemavu siku ya Jumamosi 3/12/2022 katika ukumbi wa Shule Maalumu ya Mitindo
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0718 530108
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.