Wananchi watakiwa kuondoa Hofu na kuwapeleka watoto kupata Chanjo ya Surua Rubella iliyoanza kutolewa kwa watoto wa umri wa miezi 9 hadi miaka 5 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Utoaji Chanjo hiyo katika Kituo cha Afya cha Mitindo – Misungwi amewataka Viongozi, Watendaji pamoja na Wataalam wa Afya kutoa elimu na kuhamasisha jamii na Wazazi kuwaruhusu Watoto kujitokeza kupata Chanjo ya Surua na Rubella ili kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Surua Rubella.
Mhe, Chacha amesema kwamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wazazi kuogopa na kuwa na hofu ya kupatiwa Chanjo kutokana na kuelezwa mambo tofauti kuhusu Chanjo zinazotolewa ambapo amewatoa hofu na kuwaomba wawapeleke watoto katika Vituo na maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili kupata Chanjo na amekemea Vitendo vya baadhi ya Wananchi kuamini na kupata matibabu kwa Waganga wa tiba asili waliokithiri Wilayani Misungwi.
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Emmanuel Ntibalila amesema kwamba Halamshauri ya Misungwi kupitia Wataalam wa Idara ya Afya tayari imeenza zoezi la utoaji wa Chanjo hiyo kuanzia tarehe 15 mwezi huu na zoezi litakamilika tarehe 18 ambapo wanatarajia kutoa Chanjo kwa watoto wapatao 105,410 kwa lengo lililowekwa katika Wilaya.
Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Dkt. Clement Morabu ametoa rai kwa Viongozi na Watendaji kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa Wananchi kutumia fursa hii na kujitokeza kupata Chanjo hiyo muhimu na kwa upande wa Halmashauri ya Misungwi imeandaa Vituo 142 kwa ajili ya kutoa Chanjo ya Surua Rubella ambapo Vituo vyote 59 vya kutolea huduma za Afya pamoja na maeneo mengine 85 yameandaliwa kwa zoezi hilo la Kampeni ya Kitaifa.
Wakati huo huo, baadhi ya akina mama walioleta watoto kupata Chanjo wamesema kwamba wameona umuhimu wa kuwapatia Chanjo watoto ili kuwakinga na magonjwa hayo ya Surua Rubella mara yanapojitokeza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Paulo Chacha akiwa amebeba mtoto wakati wa zoezi la utoji Chanjo ya Surua Rubella katika Hospitali ya Mitindo ambapo lengo la Kampeni hiyo kupunguza au kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Surua Rubella kwa watoto chini umri miezi 9 hadi miaka 5.
Dc Chacha akimzawadia mtoto fedha mara baada ya kupata Chanjo ya Surua Rubella katika Hospitali ya Mitindo Misungwi ambapo aliwatoa hofu Wazazi kuhusu Chanjo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.