Watahiniwa 3,274 wa Shule za Sekondari wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Sekondari wa Kidato cha Nne mwaka 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkutugenzi Mtendaji Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw, Addo Missama amesema hatua ya ufanyaji wa Mtihani wa Kidato cha Nne maandalizi ni Mazuri ambapo zoezi la kitaifa la uendeshaji wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya Sekondari la kufanikisha hatua ya kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne mwaka 2024.
Bw. Addo Missama amewataka Watahiniwa hao kufanya Mtihani wao katika hali ya amani na kuwa watulivu na kutambua kwamba Mtihani huo ni wa Taifa ambapo amewatakia afya njema wakati wote na kuwaomba wamtangulize Mungu awasaidie, sambamba na kuwaomba wasimamizi wa Mtihani kusimamia vizuri, kulingana na maelekezo na taratibu zilizotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Aidha, katika hatua nyingine Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bi. Diana Kuboja ameeleza na kufafanua kwamba jumla ya Watahiniwa 3,274 wamesajiliwa na wapo tayari kwa ajili ya kufanya Mtihani huo wa kumaliza Elimu ya Sekondari itakayofanyika mfululizo kuanzia tarehe 11/11/2024 hadi 21/11/2024 ambapo miongoni mwao Wavulana ni 1,566 na Wasichana ni 1,708 na tayari maandalizi ya msingi yapo vizuri hususani suala la usafiri kuelekea katika vituo 39 yamekamilika ambavyo ni Shule za Sekondari za Umma 32 psamoja na Shule za Sekondari 7 za Binafsi .
Akifafanua zaidi kuhusu ratiba ya Mtihani huo Bi. Diana Kuboja amesema kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania inaeleza kwamba Mitihani hiyo ya kumaliza Elimu ya Sekondari ya Kidato cha Nne mwaka 2024 itaanza siku ya Jumatatu tarehe 11 Novemba, 2024 hadi tarehe 21 Novemba, 2024 kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 9 alasiri kila siku katika masomo ya Geography, Biology, Basic Mathematics,Civics, English Language, Kiswahili, Chemistry, History, Physics, Commerce, Book Keeping, na Computer Studies pamoja na Mtihani wa Vitendo kwa masomo ya Sayansi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.