Jumla ya Watahiniwa 7,602 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi kuanzia tarehe 5 na kumaliza 6 Septemba, mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Misungwi, Bw, Ephraim Majinge kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Bw. Kisena Mabuba, alieleza kwamba Halmashauri hiyo imeshafanya maandalizi yote ya Zoezi la Kitaifa la uendeshaji wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi kwa mwaka 2018 na kwamba kuna jumla ya Watahiniwa 7,602 waliosajiliwa kwa ajili ya kufanya Mtihani wa darasa la saba ambapo Wavulana ni 3,518 na Wasichana ni 4,084.
Bw, Majinge alifafanua kuwa kati ya Watahiniwa 7,602 waliosajiliwa miongoni mwao kuna Wanafunzi 33 wenye Ulemavu wa aina mbalimbali na wenye kuhitaji mahitaji maalum wakiwemo Wavulana 16 na Wasichana 17 ambapo Watahiniwa Wasiona ni 3, wenye uoni hafifu 10, wenye ulemavu wa Masikio ni 12 (Viziwi), na wenye ulemavu wa Ngozi ni 8 (Albino) waliopo katika baadhi ya Shule za Msingi.
Afisa Elimu Majinge alisema kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ina jumla ya Shule za Msingi 145 zikiwemo Shule za Msingi za Serikali 138 na Shule za Binafsi 7 na Shule hizo zote zitakuwa na jumla ya Mikondo 357 ya Watahiniwa wote watakaofanya Mtihani huo.
Wanafunzi wa darasa la saba ktika Shule ya Msingi Kwimwa Kata ya Sumbugu wakiendelea na Masomo ya ziada wakati wa Likizo ya mwezi Juni mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi utakaofanyika kesho (Kushoto) Mwalimu akikagua Wanafunzi wakifanya majaribio ya masomo mbalimbali.
Bw, Majinge aliongeza kuwa kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania inaeleza kwamba Mtihani huo wa kumaliza Elimu ya Msingi utaanza siku ya Jumatano saa 2.00 asubuhi kwa Watahiniwa hao kufanya masomo ya Kiswahili, Hisabati na English Language na siku ya Alhamis watafanya Mtihani wa masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii .
Afisa Elimu huyo amesema kuwa Halmashauri na Wilaya kupitia Idara ya Elimu Msingi imeshakamilisha maandalizi yote ya msingi yanayohusu Usafiri na mambo mengine muhimu kwa asilimia 99 hususani suala la usambazaji wa Mitihani kutoka Makao Makuu ya Halmashauri na kupelekwa kwenye Vituo..
Bw, Majinge kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri amewataka Watumishi,Wazazi na Wananchi wote kuwaombea na kuwatakia Mitihani mwema Watahiniwa wote na mwenyezi Mungu awasaidie ili waweze kufaulu na kutimiza malengo na ndoto zao.
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Misungwi,Bw,Ephraim Majinge akifafanua na kuelezea jambo kuhusu mikakati na maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa Madiwani wa Kamati ya Huduma za Kijamii walipotembelea na kukagua katika Shule ya Msingi Busagara mapema mwaka huu.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Bw,Ephraim Majinge
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.