Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani, mshikamano na kuhakikisha wanatoa ushirikiano ili kubaini vitendo vya Uvunjifu wa amani.
Akizungumza Tarehe 22 Mei 2025 katika ziara ya kijiji cha Ibinza ambapo amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kusikiliza na kutafuta suluhu ya mgogoro wa Bwawa uliohusisha kaya moja na Wananchi wa kijiji hicho na kushughurikia kwa kusikiliza, kuongea na Wananchi pamoja na kaya husika
Pia Mhe. Samizi ameeleza kuwa Bwawa hilo limekua changamoto zinazozorotesha maendeleo ya jamii ikiwemo kukwamisha upatikanaji wa Barabara kutokana kuwepo kwa kilimo ambapo ameitaka Halmashauri ya kijiji na Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ifikapo Tarehe 28 Mei 2025 kuhakikisha wanafika kufanikisha suluhisho la mda mfupi hatimaye kupata suluhisho la kudumu ili wananchi hao waishi kwa amani.
Katika jitihada za kumaliza mgogoro huo, Mhe. Samizi ametoa maazimio mbalimbali ya utekelezaji, ikiwemo kuwataka wataalamu wa ardhi,Sheria,Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwenda katika eneo hilo ili kufanya tathimini ya Bwawa hilo ili kuendelea kulinda eneo hilo dhidi ya uharibifu.
Mhe.Samizi amesema ni muhimu kushirikiana na serikali katika kuhifadhi mazingira kwa Bwalwa hilo ni sehemu ya mazingira na kuhakikisha inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Isenengeja Bw. Selestine Shila ameshukuru kwa Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi kwa kuja kuongea na Wananchi hao ambapo Bwawa hilo limekua changamoto na kupelekea hali ya watu kuhofia usalama wao.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.