Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na Wasimamizi Wasaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Novemba 23, 2024 wameapishwa pamoja na kupatiwa mafunzo kuhusu Zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Novemba 27, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mafunzop hayo,Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo Addo Missama amewataka maafisa hao Kuhakikisha wanafuata taratibu zote za uchaguzi siku ya kupiga kura ili Kuwezesha uchaguzi kufanyika kwa Amani na utulivu.
"Jukumu hili tunapaswa kulifanya kwa uadilifu mkubwa,Tuzingatie kanuni, Sheria na taratibu za uchaguzi zinavyosema,Amani siku ya uchaguzi ipo mikononi mwetu,hivyo tuhakikishe tunatenda haki kwa kila mmoja hadi tukamilishe uchaguzi" alisema Missama na kuongeza kuwa
"Wasimamizi wa vituo pamoja na Wasimamizi Wasaidizi muhakikishe mnawahi kwenye vituo vya kupigia kura ambavyo mmepangiwa kusimamia siku ya uchaguzi ili kuweka mazingira sawa yatakayowezesha Kufanya kazi kiuweledi,
Aidha amewasisitiza Kuendelea kuhamasisha Wananchi kwenye kila kitongoji na kijiji kupitia Wazee marufuu na madhuhuri ili siku ya kupiga kura waweze kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wanaowataka kwa Maendeleo yao.
Naye Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Dickson Kawovela amewasihi na kuwaomba Wananchi wote waliojiandikisha katika Orodha ya Makazi kujitokeza na kutumia haki Yao ya Msingi na ya kikatiba ya kumchangua Kiongozi wanayempenda na kuwekeza kwamba Maandalizi yapo vizuri na wamejipanga vizuri na watahakikisha Wananchi wote wanapiga kura na kushiriki .
Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi Bi.Elly Makala ameeleza kwamba Wasimamizi wa Vituo vyote wanapaswa kuwa Waadilifu na kuzingatia Maelekezo ya Serikali na kuacha Vitendo viovu vitakavyosababisha kuingiz Vishawishi wakati wa zoezi la Uchaguzi na kuwataka kuwa waaminifu na waendelee kumcha Mwenyezi Mungu.
Zoezi la upigaji kura litafanyika nchini siku ya Jumatano Novemba 27 Mwaka huu kuanzia majira ya saa mbili kamili za asubuhi hadi saa 10 za Jioni kwenye vituo vya kupigia kura vilivyopo kila kijiji.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.