Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda akabidhi mabati 108 yenye thamani ya shilingi Milioni 2. 8 kwa ajili ya kupaua vyumba viwili vya Madarasa ya Sekondari mpya yaliyojengwa na Wananchi katika Kijiji cha Gambajiga, Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gambajiga katika eneo la Ujenzi wa Sekondari hiyo, Juma Sweda amewataka Wananchi hao kueezeka haraka madarasa hayo mawili na kukamilisha na mengine ikiwemo Jengo la Utawala na kuwahakikishia kwamba Shule hiyo mpya ya Sekondari inafunguliwa mwezi Januari mwaka 2021, ambapo amewaomba kuchapa kazi na kukamilisha ujenzi huo mapema ili Wanafunzi waanze kunufaika na kupata elimu karibu.
Juma Sweda amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Gamabajiga Kata ya Kanyelele kwa juhudi na kazi kubwa waliyoionyesha kwa kuanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari, lengo ikiwa ni kuongeza na kupandisha kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Misungwi na kuondoa adha kwa watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule na Serikali itatoa Walimu mara baada ya shule kufunguliwa rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi , Kisena Mabuba amesema kwamba Halmashauri kwa kutambua juhudi na kazi kubwa iliyofanywa na Wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya Sekondari hiyo, wameamua kuunga mkono na kushirikiana nao kwa kuwapatia mabati 108 ambayo ni bando tisa zenye thamani ya shilingi Milioni 2.8 hata hivyo wataendelea kutoa mchango na kushirikiana na Wananchi kwa kila hatua.
Amesema kwamba Halmashauri inatekeleza maagizo na maelekezo ya Mhe, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye ameagiza Wanafunzi wote watakaochaguliwa kufikia tarehe 28 mwezi Februari mwakani waanze masomo haraka hivyo mikakati na juhudi zinaendelea kufanyika kwa kila Kata kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vinavyopungua na kukamilisha ujenzi wa shule mpya ili Wanafunzi waweze kusoma.
Ameongeza kwamba Viongozi wa ngazi ya Wilaya wameamua kuungana na Wananchi wa Gambajiga kufanya kazi katika sikukuu ya Uhuru na wameshiriki pia kupanda miti katika maeneo ya Shule na kuweka vifusi katika msingi wa vyumba vya madarasa ili kutekeleza adhima ya Serikali ya Hapa kazi tu na wtaendelea kuwashika mkono na hatimaye kukamilisha ujenzi huo hadi Wanafunzi watakapoanza masomo mwakani.
Awali akielezea namna Wananchi walivyoshiriki katika ujenzi wa vyumba 4 vya madarsa, Jengo la Utawala na ofisi ya Walimu, Choo ambavyo mbaoma yamekamilika pamoja na kuanzisha vyumba vingine vya madarasa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Gambajiga Jeremiah Njilima amesema kwamba Wananchi hao waliopo kwenye Kaya 447 waliamua kuanza ujenzi huo mwezi Agosti mwaka huu 2020 kwa kuchangia mchango wa shilingi elfu 50 kila Kaya kwa awamu mbili ambapo wamefanikiwa kujenga vyumba hivyo na kufikia hatua ya boma.
Baadhi ya vyumba viwili vya Madarasa vimekamilika kwa hatua ya boma na matarajio ni kueezeka na kukamilisha tayari kwa ajil ya kufunguliwa mwezi Januari mwaka 2021 kwa Shule ya Sekondari Gambajiga Kata ya Kanyelele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Kisena Mabuba akipanda mti katika maeneo ya Shule mpya ya Gambajiga katika Sikukuu ya Uhuru mwaka 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gambajiga (walnaonekana pichani ) wakati wa kukabidhi mabati 108 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari hiyo amabyo imejengwa kwa nguvu na michango ya Wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.