Msimamizi wa Uchaguzi wa Uchaguzi wa Jimbo la Misungwi,katika Halmashauri ya Wilaya,Eliurd Mwaiteleke ametangaza Matokeo ya uchaguzi wa Udiwani katika Kata ya Kijima ambapo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM kuibuka Kidedea.
Mwaiteleke alitangaza Matokeo hayo ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani uliofanyika katika Kata ya Kijima ambapo Mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Kanzaga E.Katamki ameibuka Kidedea.
Mwaiteleke alitangaza Matokeo hayo ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani mara baada ya kukamilika kwa Zoezi la Upigaji Kura pamoja na kuhesabu hivyo kwa Mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2015,alitangaza rasmi kwamba Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM,Kanzaga E.Katamki ameshinda kwa kupata Kura 1,428 akifuatiwa na Mgombea wa Chama cha CHADEMA,Gabriel M.Shiloti aliyepata Kura 614 na Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo,Elius J.Mayeka alipata Kura 205.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Misungwi alieleza kwamba katika Uchaguzi huo Idadi ya Wapiga Kura walioandikishwa ni 4,578,Idadi halisi ya Waliopiga Kura ni 2,366,na Idadi ya Kura Halali zilizopigwa ni 2,307 na Idadi ya Kura zilizokataliwa ni 59.
Mwaiteleke alisema kuwa Zoezi la Upigaji Kura limefanyika vizuri kwa amani na usalama ambapo Vituo vya Kupigia Kura vyote 12 vilifunguliwa saa 1.00 asubuhi na Wananchi walijitokeza kupiga Kura kwa wingi hadi Vituo vinafungwa saa 10.00 jioni hali kwa ujumla ilikuwa nzuri na utulivu wa kutosha.
Alibainisha na kuvitaja Vituo vyote 12 vilivyotumika kupiga Kura ambavyo ni pamoja na Chande Mwembeni,Shule ya Msingi Ikoma,Mashineni Igobeko 1,Shule ya Msingi Isakamawe -1,Shule ya Msingi Isakamawe -2,Kijima Ofisi ya WEO,Shule ya Msingi Kijima "A"-1,Shule ya Msingi Kijima "B'-2, Shule ya Msingi Kijima "B"- 1,Mwamaguha Chama cha Ushirika -1,Mwambola Mkwajuni -1,Shule ya Msingi Mwamaguha .
Kwa Mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo iliitisha kufanyika kwa Uchaguzi huo Mdogo wa Udiwani kwa nchi nzima tarehe 26 Novemba,2017 kwa ajili ya kuziba Nafasi zilizokuwa Wazi za Madiwani katika Kata 43 kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo Kifo,Kuondolewa Madarakani pamoja na Kuvuliwa Uanachama wa Chama na kukosa sifa ya kuwa Kiongozi.
Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Kijima katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi umefanyika ikiwa ni kutokana na kufariki Dunia kwa aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Marehemu, Nkwabi Mpanduji mnamo mwezi Julai 2017.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.