Kampuni ya DOWEICARE TECHNOLOGY LTD yatoa msaada wa taulo za kike aina ya soft Care Sanitary pad kwa wanafunzi wa kike 10,008 wa shule za Sekondari na Msingi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Viwanja vya Shule Sekondari Misungwi, Balozi wa Sott care nchini Zarina Hassan maarufu “Zari the Boss Lady” amesema msaada huo umetolewa kwenye shule za sekondari 32 na shule za Msingi 150 ili waweze kujiamini pindi wanakuwa katika hedhi na kuitaka Serikal kuanzisha na kulikuchukulia suala hili kipaumbele na kuwa Kampeni ya Kitaifa ya ugawaji wa Taulo kwa Wanafunzi wa kike nchi nzima.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuona umuhimu wa kununua taulo za kike pindi wanapofanya mahitaji ya watoto wao ya shule waache kutumia vitambaa wakati wa hedhi kwa sababu wakivaa muda mrefu hutoa harufu mbaya na kusababisha kukosa raha na kusababisha kushindwa kusoma .
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ,Victor Zhang ameishukuru sana shule ya Misungwi kwa kupokea misaada yao na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na Serikali kutoa misaada ya taulo za kike,ikiwa ni sehemu ya wao kurudisha shukrani kwa jamii
Bw. Victor Zhang amesema kwamba Kampuni imeweza kusaidia Halamshauri ya Misungwi kwa kutoa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 13 kwa ajili ya Wanafunzi wote wa kike wa shule 32 za Sekondari za Serikali na 7 za Binafsi pamoja na baadhi ya Wanafunzi wa shule za msingi.
Naye, Mwanafunzi wa shule ya Misungwi Sekondari Sabrina Yahya akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema kutumia taulo hizo kuna faida kwani humfanya msichana kuwa na amani wakati wa hedhi na kuwa msafi na huru muda wote.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya taulo hizo iliyofanyika katika Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel ambaye alikuwa mgeni rasmi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo wa taulo za kike kwenye shule mbalimbali zikiwemo za msingi na Sekondari Misungwi,Elpase,Jitihada,Zulu,Igokelo,Aimee Mirembe na kuziomba taasisi zingine zijitokeze kusaidia wanafunzi na kuelekeza kwamba suala la ugawaji wa Taulo kwa Watoto wa kike iwe Kampeni maalumu ya kunusuru na kuwakomboa watoto wa kike.
Mhandisi Robert Gabriel pia aliagiza Halmashauri ya Wilaya kuweza kutoa eneo la kiwanja kwa ajili ya ujenzi na uwekezaji wa Kampuni ya Doweicare
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ,Selema Ikowelo ,amsema ukosefu wa taulo za kike imekuwa tatizo kubwa sana kwa wanafunzi wengi katika Wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Mhe,Robert Gabriel akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Misungwi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronica Kessy akimkabidhi tuzo ya heshima Zarina Hassani katika zoezi la ugawaji wa Taulo za kike katika viwanja vya Sekondari Misungwi.Akishuhudiwa mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya(mkono wa kulia) pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi(katikati)Petro Sabato
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Misungwi wakipokea msaada wa Taulo za kike katika viwanja vya Misungwi Sekondari Wilayani Misungwi.
Zarina Hassani alimaarufu kwa jina la " Zari The Boss Lady" akizungumza katika hafla ya ugawaji wa taulo za kike katika viwanja vya Misungwi Sekondari.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.