Jumla ya Watahiniwa 2,448 wanatarajiwa kuanza Mitihani ya Kidato cha Nne leo tarehe 4 mwezi Novemba 2019 na kukamilika tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu 2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi, Dianah Kuboja amezungumza leo na Mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw, Kisena Mabuba ambapo amesema kwamba Idara ya Elimu Sekondari pamoja na Viongozi wa Wilaya wameshafanya maandalizi yote vizuri ya zoezi la uendeshaji wa Mitihani hiyo ya kuhitimu Elimu ya Sekondari kwa mwaka 2019 na taratibu zote zimeshakamilika na Watahiniwa wote wapo tayari na wameandaliwa kikamilifu kupitia mada za masomo yote.
Baadhi ya Wnafunzi wa Shule ya Sekondari Misungwi iliyopo Mjini Misungwi wakiwa katika kikao maalum na Walimu wao ikiwa ni kwa ajili ya kuwaasa na kuwajenga Kisaikolojia ili kukabiliana na Mitihani ya mwisho wa masomo yao mwaka 2019.
Bi, Dianah Kuboja ameeleza kuwa Halmashauri ina jumla ya Watahiniwa 2,448 waliosajiliwa kwa ajili ya kufanya Mitihani hiyo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2019 ambapo watahiniwa hao watafanya Mitihani yao hiyo katika Shule za Sekondari 26 kati ya Shule za Sekondari 30 za Halamashauri ya Wilaya ya Misungwi ambazo kati ya hizo Shule 23 ni za Serikali na Shule za Sekondari 3 ni za binafsi.
Afisa Elimu huyo ameongeza kwamba kwa mujibu wa ratiba ya Mitihani hiyo iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa kuwa kwa Watahiniwa hao watafanya Mitihani ya masomo kumi na moja yaliyogawanyika katika masomo ya Sanaa, Sayansi na Biashara na Mitihani hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 4 mwezi Novemba mwaka huu 2019 kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kila siku ukiondoa siku ya Jumamosi na Jumapili hadi tarehe 20 mwezi Novemba 2019.
Bi, Kuboja amewataka Watahiniwa hao kuwa watulivu na waelevu na kuwa waaminifu wakati wote wa Mitihani na kumtanguliza Mungu mbele na akawe msaada mkubwa kwao na kuwatakia kila kheri na mafanikio pamoja na kuwa na Afya njema wakati wote wa Mitihani yao.
Aidha, Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya Mitihani ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne ambapo kwa mwaka 2018 ilikuwa katika nafasi ya tano (5) kimkoa kati ya Halmashauri nane (8) za Mkoa wa Mwanza .
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.