Walengwa wa Mpango wa Tasaf wa Vijiji Vinne vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wapatiwa Mafunzo ya uundaji wa Vikundi vya kuweka Akiba na kukopa kwa ajili ya kukuza uchumi katika Kaya Maskini.
Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku mbili kwenye Vijiji vya Lubuga,Iteja,Ngudama na Nyang'homango na Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima na Misungwi ambayo yalilenga kuwajengea uwezo Walengwa wakuweza kuunda Vikundi vya kuanzia Watu 10 hadi 15 vya kuweka Akiba na kukopa ili kukuza uchumi wa Wananchi kupitia shughuli za Miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha Mazo ya biashara,Kilimo cha Bustani ya mbogamboga na matunda,Ufugaji na Ushonaji.
Akizungumza mara baada ya Mafunzo hayo,Ndugu,Lucas Gwabo Mkazi wa Kijiji cha Iteja alisema kwamba mpango huu utawanufaisha Wananchi hususan Walengwa wa Mpango wa TASAF kwa kuwainua kiuchumi kupitia uwekaji wa Akiba na kukopa katika Vikundi kwa lengo la kutekeleza miradi ya Kilimo na Ufugaji na kuwaongezea kipato Wananchi.
Kwa upande wake Bibi Stella Kihombo ambaye alikuwa Mwezeshaji wa Kitaifa kutoka Manispaa ya Ilala alieleza kwa Wananchi fursa za kiuchumia ambazo ni pamoja na ufugaji wa kuku,kitaalamu,Kilimo cha mbogamboga na matunda,Kilimo cha Mazao ya biashara ikiwemo Mpunga na Dengu pamoja na Wanawake kuweka akiba kupitia bajeti ya feadha za matumizi ya nyumbani na kusisitiza Walengwa wawezeshwe ili kuzitambua fursa hizo na hatimaye waweze kujiunga katika Vikundi na kuinua uchumi katika Kaya.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.