Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na Elimu, watendaji wa kata na wakuu wa idara wapatiwa mafunzo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Hayo yamebainishwa tarehe 5 Disemba 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama wakati Akifungua kikao cha maelekezo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vituo vya kutolea huduma za afya na elimu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo ameeleza kuwa bila ya maadili mema na uwazi katika utendaji wa shughuri za Kiserikali ni vigumu kufikia malengo ya maendeleo endelevu ambavyo kila mmoja katika Serikali anawajibika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kwa njia inayofaa na kwa manufaa ya wananchi wote.
Naye Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Misungwi Bi. Elly Makala amesema kuwa kuelekea maadhimisho ya siku kuu ya Maadili tarehe 10/12/2024 kuna umuhimu wa kuimarisha maadili katika utendaji wa majukumu ya kiserikali na jamii ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za maadili katika kazi zao ili kujenga imani na uaminifu kutoka kwa wananchi katika kufanikisha ukamilishaji wa miradi ya kimaendeleo..
Bi. Elly ameongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa kila mtu kuchukua hatua za katika kupambana na rushwa na kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa katika kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano na uwajibikaji katika sekta mbalimbali ikiwemo za afya na elimu.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Misungwi Bi. Piniel Titto amesema kuwa Kikao hicho kimelenga pia kujadili mikakati ya kuboresha huduma za afya na elimu ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila ya ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, wananchi na wadau mbalimbali.
Afisa ugavi wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Andrew Ndaki amewataka Watendaji wa kata,Walimu na Wahudumu wa afya kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi na utekelezaji wa miradi ngazi ya serikali za vijiji na vitongoji kuhakikisha wanakuwa makini katika ufatiliaji wa manunuzi na usimamizi wa miradi katika kata zao.
Baadhi ya Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na elumu na watendaji wa kata watoa pongezi kwa kupata kikao hicho ambapo kitakua msaada katika kufanya kazi kwa weledi na kuyatekeleza yale yaliotolewa na kuelekezwa kaitika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanasimamia kwa weledi manunuzi ya yanayohitajika Katika miradi.
Kikao hicho kiliudhuriwa na Maafisa Takukuru ngazi ya Wilaya ,Wakuu wa idara Halmashauri ,Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na elumu na watendaji wa kata.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.