Halmashauri ya Misungwi imetoa mafunzo ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa Planrep ulioboreshwa na mfumo wa FFRAS kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Maafisa Wasaidizi katika Idara zote za Halmashauri ili kuwawezesha kuandaa na kutuma taarifa za mpango wa Bajeti na Makusanyo ya Fedha za Halamashauri TAMISEMI kwa haraka na urahisi zaidi.
Mafunzo hayo yametolewa kuanzia tarehe 18- 22/9/2017 na Wawezeshaji ambao ni Afisa Mipango,Mweka Hazina,Mganga Mkuu, Katibu wa Afya na Mchambuzi wa Mifumo wote wa Halmashauri mara baada ya awali kupewa mafunzo yaliyotolewa na PS3 mapema mwezi Agosti 2017 Jijini Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutumia Teknolojia ya kisasa katika uaandaaji na utumaji wa taarifa.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.