Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania tawi la Mwanza wafurahishwa na kupongeza shughuli za utekelezaji wa miradi mbalimbali zinazofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Ujenzi wa Jengo la Upasuaji ukiendelea katika hatua za ukamilishaji katika Kituo cha Afya cha Mbarika kwa gharama ya Tsh, 203,000,000/= za ufadhili wa Mradi wa Mama na na Mtoto.
Wajumbe hao walitoa pongezi hizo wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi iliyofanyika hivi karibuni ambapo Mwenyekiti wa ALAT Mkoa, Mhe, Hilali Elisha alisema kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imetekeleza miradi hiyo kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana na itaweza kusaidia na kunufaisha Wananchi wa maeneo husika kwa kupata huduma safi na salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke alisema Jumuiya ya ALAT Mkoa imeweza kutembelea na kuona miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Mashine ya kukamua Alizeti ya Kikundi cha Madelelya ,Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi katika Sekondari ya Aimee Milembe,Ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya cha Misasi,Ujenzi wa vyumba vitatu vya Madarasa ya Kidato cha tano na sita na ukarabati wa Madarasa katika Shule ya Sekondari ya Misasi, Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Walimu (six in one) katika Shule ya Sekondari Isakamawe ,mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa,choo na Kisima cha maji katika Shule ya Msingi Buhingo, Ujenzi wa Madarasa na Jengo la Utawala katika Shule mpya ya Sekondari ya Gulumungu, Mradi wa ujenzi wa Jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mbarika pamoja na kutembelea chanzo cha maji cha KASHWASA eneo la Ihelele.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.