Wajumbe wa Bodi ya mpango wa TASAF Taifa wameipongeza Halmashauri Wilaya ya Misungwi kwa kutimiza na kutekeleza kikamilifu mpango wa kunusuru kaya masikini awamu ya tatu kwa kutoa shilingi milioni 22,073,234/= kwa Vikundi vitano pamoja na shilingi Milioni 342,323,000/= za Uhaulishaji Wananchi wa Kijiji cha Igenge Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Hayo yamebainishwa Januari 16, 2025 na Kiongozi wa Bodi yampango wa TASAF Taifa Bw. Naftali Ng’umi wakati wa ziara ya kutembelea vikundi 5 vyenye jumla ya wananchama 69 katika Kijiji cha Igenge Kata ya Mbarika vilivyopewa nafasi ya kuibua miradi kwa kila kikundi ambapo ameridhishwa na kupongeza jitihada zinazofanywa na wanakikundi hao kwa ajili ya kuwanufaisha kiuchumi ambapo fedha walizopokea kwa mwaka 2023/2025 zimekuea sehemu ya kuwawezesha kuwapa vifaa mbalimbali vya utengenezaji wa batiki.
Naye Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amewapongeza wanakikundi kuinua vipato vya familia zao kwa kujipatia mitaji ya kuanzisha miradi midogo midogo, kupitia programu ya vikundi vya TASAF na wamethibitisha kuwa, licha ya kupokea fedha lakini pia walijengewa uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa kupitia fedha za ruzuku wanazopokea.
Kwa upande wake Afisa ufuatiliaji wa TASAF Wilaya Bw. Steven Samwel amesema kuwa vikundi hivyo vilipokea elimu kutoka kwa watalamu waliwajengea uwezo wa kuanzisha vikundi vya kuwekeza pesa kutokana na ruzuku wanayoipa kutoka TASAF,na bada ya kuanzisha vikundi hivyowameweza ambapo biashara hizo zimepunguza ugumu wa Maisha na kuwekeza, kukopa na kurejesha kwa wakati, na kuongeza ujuzi wa kiujasiriamali.
Bw. Steven Samwel ameeleza kuwa vikundi hivyo vilivyonufaika na mpango huo ni pamoja na kikundi cha amani- utengenezaji wa vikapu wanachama 12, kikundi cha mlimani city- utengenezaji wa batiki wanachama 13,kikapu ushirikiano- utengenezaji sabuni wanachama 15 ,kikundi cha baraka -ufugaji kondoo wanachama 15 pamoja na kikundi cha umoja ni nguvu -ufugaji kondoo wanachama 14 waliofanikiwa kuhudumia familia, kuboresha makazi , kujihusisha na biashara ndpgpndogo, kilimo na Ufugaji na kupata uwezo katika kaya hizo.
Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Mlimani City kijiji cha igenge kata ya Mbarika Bi. Kamuli Charles ameishukuru Serikali ya awamu sita kwa kuwawezesha na kuwapatia mradi kupitia vikundi ambapo ameeleza kuwa Hapo mwanzo hatukuamini kama jambo hili kama litawezekana, kutoka na kiasi cha pesa tunachopokea, lakini tuna mfuko wa jamii ambao tunasaidiana kutatua changamoto za kijamii kama msiba na ugonjwa, kwa kupata faida ya 108,000/= kupitia biashara, inayotuwezehsa kuendelea kuweka akiba, kukopa na kupata marejesho, huku faida ya biashara ikituwezesha kuhudumia famialia zetu pi wamepata ujuzi wa kutengeneza batiki ,hivyo itasidia kupata kipato cha kuweza kukidhi mahitaji katika familia zao.
Mpango wa Kunusuru kaya masikini, wenye lengo la kukuza pato la familia, umekuwa na programu ya vikundi vya kuweka na kuwekeza kwa walengwa walio kwenye mpango ili kukuza uchumi wa kaya kwa muda mrefu sasa ambapo katiKA Ziara hiyo na iliyoambatanisha na kujumuisha Wataalam mbalimbali kutoka ngazi ya Taifa na Mkoa wa Mwanza.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.