DC Misungwi awataka Wahitimu 65 wa mafunzo ya Jeshi la Akiba mwaka 2024 kuchangamkia fursa za Mikopo ya Vijana ili kuinua kipato na uchumi wa familia katika Halmashauri Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe. Samizi amebainisha hayo wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa Wahitimu 65 siku ya Jumatano tarehe 30 Oktoba, 2024 yaliyofanyika takribani miezi 4 katika Tarafa ya Usagara ambapo wamejifunza ujasiriamali, ukakamavu pamoja na kwata, matumizi ya silaha, Usalama wa raia, kuzuia na kupambana na rushwa, huduma ya kwanza, Utimamu wa mwili na kuwasihi kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili kuleta tija katika jamii na kuwa mfano mzuri wa uongozi na uwajibikaji katika uwezo wa kushiriki katika shughuli za ulinzi na usalama, kwa manufaa ya nchi na kujiepusha na vitendo vya uhalifu hivyo ni muhimu kwao kutumia maarifa hayo kwa njia sahihi.
"Mmefuzu na mnatambulika rasmi kama mlivyo kula kiapo nendeni mkakiishi, mkakisimamie kama mlivyofundishwa na muwe mfano bora katika jamii". Alisisitiza Mhe. Johari Samizi.
Mhe. Johari Samizi amewaeleza Wahitimu hao kwamba wanapaswa kuungana na vyombo vya usalama katika juhudi za kupambana na uhalifu na kuimarisha amani katika Wilaya ya Misungwi ambapo kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha usalama wa jamii na kutoa ushirikiano wa dhati na ni muhimu kufanya kazi kwa kujituma samabamba na kutumia vizuri fursa za ujasiriamali kwa kujiunga kwenye Vikundi kwa lengo la kupatiwa Mikopo ya Vijana na kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Naye Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Misungwi Bw. Alexander Magukura akieleza namna mafunzo yalivyoendeshwa na Wakufunzi kuanzia mwezi Julai 2024 katika Tarafa ya Usagara maeneo ya Sanjo ambapo kupitia vijana 89 walioanza mafunzo walifundishwa mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya silaha, Usalama wa raia, kuzuia na kupambana na rushwa, Uzalendo, huduma ya kwanza, utimamu wa mwili na ukakamavu ambapo baadhi yao hawakuweza kuhitimu mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali kama vile utoro na nidhamu, hivyo hadi kuhitimishwa kwa mafunzo hayo vijana 65 pekee ndio wanefanikiwa kuhitimu.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo, Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalam na Watendaji wa Serikali, Maafisa wa Jeshi la Ulinzi, Wazazi, na wanajamii, ambapo Mhe. Samizi alihimiza umuhimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba katika kujenga taifa lenye usalama na maendeleo endelevu.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.