• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Wafugaji watakiwa kusajili mifugo Wilayani Misungwi

Imewekwa : September 9th, 2022

 

Mkuu  wa  wilaya  ya  Misungwi  Mhe, Veronica  Kessy  amewataka  wafugaji  kusajili  mifugo  kuongeza  thamani  ya  nyama  ndani  na  nje  ya  nchi.

Mkuu  wa  Wilaya  hiyo  amewataka  wafugaji  hao  kusajili  mifugo  yao  kwa  wakati  kama  sheria  inavyowataka  ya  utambuzi, usajili  na  ufatiliaji  wa  mifugo  sheria  namba   12  ya  mwaka  2010.

Ameyasema  hayo  mapema  wiki  hii  alipotembelea  eneo  la  mnada  wa  upili  uliopo  kijiji  cha  ng’ombe  Kata  ya  Igokelo  ambapo  zoezi  hilo  lilizinduliwa  tarehe  7 september 2022  Wilayani  Misungwi  na  kitaifa  zoezi  hilo  lilizinduliwa  na  Waziri  wa  mifugo  na  uvuvi  Mhe, Mashimba  Ndaki  mwezi  Agosti, 2021  na  sasa  linaendelea  nchi  nzima  na  mwisho  wa  zoezi  hili  kitaifa  ni  tarehe  30, September, 2022.

Aidha Bi. Veronika  Kessy  amesema  kuwa  utambulisho  wa  mifugo  ni  uwekaji  wa  alama  au  utoaji  majina  ya mifugo  kwa  kufuata  mfumo  na  utaratibu  uliokubalika  kisheria  katika  nchi  na  kimataifa.

 “Alama  hizi ni  kwa  ajili  ya  kufahamu  mifugo,umiliki  wake  maeneo  inatoka  au  inapofugiwa” alisema  mkuu  wa  wilaya  ya  Misungwi.

Hata  hivo  aliwataka  wafugaji  kuona  umuhimu  wa  kusajili  mifugo  yao  kwa  kufanya  hivyo  wataweza  kutambua  mifugo  ilipo  na  umiliki  wake,  uhakika  wa  soko  na  mazao  yake  ndani  na  nje  ya  nchi  na  kuwezesha  serikali  na  wadau  kuweka  mipango  madhubuti  ya  kuboresha  huduma  kwa  mifugo  madhubuti  ya  kuboresha  huduma  kwa  mifugo  pamoja  na  kudhibiti  wizi  wa  mifugo  na  kuwezesha  bima  na  mikopo  kwa  wafugaji.

Katika  ziara  hiyo  DC alifafanua  kuwa  kwa  mfugaji  atakayeshindwa  kusajili  mifugo  yake  kufikia  tarehe  30 September  2022  atashindwa  kusafirisha  wala  kuuza  mifugo  yake  mahali  popote  na  kuchukuliwa  hatua  za  kisheria  na  kutozwa  faini  isiyozidi  milioni  mbili  au  kwenda  jela  mwaka  mmoja  au  vyote kwa  pamoja.

 Kwa  upande  wake  Afisa  kilimo  na  uvuvi  Dkt. Crispine  Laurence Shami  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Misungwi  amesema  katika  zoezi   hilo  la  utambuzi  na  usajili  wa  mifugo  wamejipanga   kuvalisha  mifugo  takribani  341,000  ikiwemo  ng’ombe,  mbuzi, kondoo  na  punda  ambapo  zoezi  hilo  linaendelea  mpaka  mwishoni  mwa  September, 2022. 

Dkt. Shami  amefafanua  kampeni  ya  uzinduzi  huo  ni  kwa  ajili  ya  kuendana  na  tamko  la  Serikali  la  kuhakikisha  kwa mifugo  yote  inatambuliwa  na  kusajiliwa  kwa  kuvalisha  hereni  ili  kukidhi  matakwa  ya  kitaifa  na  kimataifa, Dkt. Shami  amewashauri  wafugaji  kusajili  mifugo  yao  ili  kukidhi  matakwa  ya  kimataifa  ya  mifugo  hiyo  na  hasa  nyama  ili  kusafirisha  nje  na  kukidhi  viwango  vya  kimataifa  na  kudhibiti  wizi  wa  mifugo  ambao  ulikuwa  umekithiri  kwa  kiwango  kikubwa.

Naye  mwenyekiti  wa  wafugaji  mkoa  wa  Mwanza Bw, Mathias  Kitangwa  ameishukuru  Serikali  ya  awamu  ya  sita  kwa  kuwaona  wafugaji  ambapo  sasa  mfugaji  anakopesheka  na  kuaminika  na  benki  kupitia  mifugo  yao.

“Sasa  hivi  tunakopesheka  mabenki  yanatuamini,  mnyonge mnyongeni  lakini  haki  yake  mpeni” Alisema  Bw.Kitanga.

Bw.Kitangwa  amesema  zoezi  hilo  lina  faida  kwao  kwani  litawasaidia  kudhibiti  wizi  wa  mifugo  ambapo  mifugo  hiyo  itakuwa  imesajiliwa  kwenye  mfumo.

Mkazi wa kijiji  cha  ng’ombe  Bw. Wilson  Masanja  aliomba  Elimu  iendelee  kutolewa  kwa  wafugaji  juu  ya  zoezi  la  uvalishaji  hereni  kwa  mifugo  ili  kutambua  faida  na  hasara  endapo  hawatasajili  mifugo  hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronika Kessy akikata utepe katika uzinduzi wa usajili wa Mifungo kwa kuvalisha hereni katika Mnada wa Upili uliofanyika katika kijiji cha ng'ombe Kata ya Igokelo tarehe 7,Septemba 2022.

Afisa Kilimo Bw,Philemon Katabazi akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa usajili wa Mifugo kwa kuvalisha hereni ambapo zoezi hilo liliongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronika Kessy katika Mnada wa Upili Kata ya Igokelo.

Baadhi ya Wafugaji na Wataalamu waliohudhuria katika Uzinduzi wa Usajili wa Mifugo katika mnada wa Upili kata ya Igokelo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Veronika Kessy ambapo zoezi hilo nimezinduliwa tarehe 7,Septemba 2022

Matangazo

  • SHULE ZILIZOVUNJA REKODI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 February 01, 2025
  • TANGAZO ZABUNI UPANGISHAJI VIBANDA VYA HALMASHAURI MWAKA 2023/2024 June 28, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 20, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE WA JIMBO LA MBARALI NA MADIWANI KATIKA KATA SITA ZA TANZANIA August 10, 2023
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • DC Misungwi awataka Wananchi wa Kijiji cha Ibinza kata ya Isenengeja kudumisha amani na mshikamano.

    May 22, 2025
  • DC Misungwi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kukwa Shule za msingi 16.

    May 21, 2025
  • Misungwi yapongeza kwa upatikanaji wa Mitambo ya kuondoa magugu maji itakayowasili mwishoni mwa mwezi julai 2025

    May 19, 2025
  • DC Misungwi awapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Asilimia 99.75

    May 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi: 0717259106

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.