Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Mwanza azindua ujenzi wa Vyumba 24 vya Madarasa Shule ya msingi Mbela Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Mhandisi Robert Gabriel ameungana na Wananchi mapema hapo jana 25,07,2022 katika kuchimba Misingi ya ujenzi wa Madarasa 24 katika viwanja vya shule ya Msingi Mbela ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Kampeni kubwa ya Kizalendo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa kwa Shule za Misingi na Sekondari Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Wananchi ,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Mhandisi Robert Gabriel amesema kampeni kubwa ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ni matokeo na ushirikano wa viongozi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuwaweka watoto katika mazingira rafiki ya kujifunza na kujifunzia na kwamba kazi hiyo itafanya kwenye kila Halmashauri zikigharimu Bilioni 230 kwa Madarasa 11904.
Mhe,Mhandisi Robert Gabriel ameongeza kuwa serikali pamoja na nguvu za Wananchi madarasa 52 yatajengwa na kuondoa adha ya msongamano kwa watoto kukaa chini na wanapokaa chini hawezi kuandika vizuri.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel amekemea vikali kwa yeyote ambaye atathubutu kutumia fedha ya umma hata mfumbia macho na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu pamoja na kupelewa mahakamani,sambamba hilo amezitaka Halmashauri kuongeza bidii katika ukusanyaji wa mapato.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Veronika Kessy amesema kuwa changamoto ya upungufu vyumba vya wa madarasa bado ni kubwa katika Shule za Msingi Wilaya ya Misungwi hivyo kwa Ujenzi wa vyumba vya madarasa utaondoa adha ya Wanafunzi kukaa kwa wingi katika madarasa.
Bi,Veronika Kessy amefafanua katika Kauli ya Mbiu Uzalendo Kwanza Kazi Iendelee imeleta mafanikio makubwa ambayo inawataka Wananchi kujitolea katika hali na mali kuleta maendeleo na amewashukuru Wananchi na Wadau mbalimbali kwa kujitokeza kwa wingi katika Uzinduzi wa Ujenzi wa Vyumba vya madarasa 24 katika Shule ya Msingi Mbela.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Gabriel kwa mwitikio wake wa kuja Misungwi kuungana wa Wananchi katika uzinduzi na uchimbaji wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Mbela;na Madarasa hayo yatakapokamilika yatasaidia kuondoa changamoto ya Wanafunzi kurundikana kwa wingi katika madarasa.
“Nashukuru sana kwa niaba ya Wananchi kwa jinsi ulivyokuwa mbunifu na mchapa kazi na kuliona jambo hili na kulifanyia kazi kuja kuzindua hivi vyumba vya madarasa 24 katika Shule Msingi Mbela.”
Philipo Manumbu ,Mwenyekiti wa Kitongoji wa Kitongoji cha Misri amesema kuwa katika kijiji cha Mbela kuna uhaba wa Shule za Msingi katika vitongoji sita kuna shule moja tu na hivyo kupelekea mrundikano mkubwa wa wanafunzi katika Shule ya Mbela,hivyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na Wananchi kwa kuanzisha ujenzi wa vyumba madarasa na kwamba baada ya Uzinduzi huo mchakato ujenzi utakuwa endelevu.
Mkazi wa Kitongoji cha Mbela B Bi,Leticia amefafanua kuwa ana furaha kubwa kwa kampeni hiyo ya Ujenzi wa Vyumba vya madarasa huku akibainisha kuwa awali palikuwa na changamoto ya madarasa hali iliyosababisha wanafunzi kuwa na zamu kwa wiki wakienda asubuhi na inayofuata wakiingia mchana.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.