Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yaanza zoezi la kuhakiki Kaya maskini zaidi ya 8,566 kwa mfumo wa Kieletroniki kwa ajili kupata idadi halisi ya Kaya maskini zitakazonufaika katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mpango wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba alisema kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa Watendaji watakaojihusisha na na udanganyifu kwa kuingiza Kaya na watu wasio na sifa na kuwataka wafanye kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa.
“ Katika zoezi hili umakini na weledi wa Watendaji ndio unatakiwa kwa lengo la kuondoa na kutokomeza walengwa hewa na kuwaonya wale watakaoshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na endapo itabainika kutokea kwa udanganyifu ama uzembe wowote watashughulikiwa kikamilifu ,” alisisitiza Mabuba.
Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Wilaya ya Misungwi, Steven Samweli alisema na kueleza kwamba katika zoezi la uhakiki huo wanatarajia kuzifikia Kaya maskini zipatazo 8,566 zilizomo katika vijiji 60 kati ya vijiji vyote 114 vya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, na kwamba katika mpango huu wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu vijiji vyote 114 vitanufaika na mpango huo wa TASAF.
Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya taifa, Grace KIbonde alisema kuwa mpango wa TASAF awamu ya tatu umechangia sana katika kuchagiza maendeleo ya kiuchumi hapa nchini na kueleza kuwa kaya za walengwa zimewezeshwa kiuchumi kwa kuinua kipato kupitia shughuli za ufugaji, kilimo, uvuvi na shughuli za ujasiriamali na hatimaye walengwa wameweza kujikomboa na kupata maisha bora.
Baadhi ya Wawezeshaji wa ngazi ya Wilaya ya Misungwi wakimsikliza Mwezeshaji wa TASAF ngazi ya taifa wakati wa mafunzo kwa ajili ya maandalizi ya zoezi la kuhakiki Kaya maskini katika Wilaya ya Misungwi hivi karibuni.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.