Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,imepokea Kivuko kipya cha MV MWANZA kwa ajili ya kuboresha huduma za Usafiri wa abiria na Mizigo katika Vivuko vya Kigongo Wilayani Misungwi na Busisi Wilayani Sengerema .
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi Issack Kamwele amepokea Kivuko hicho rasmi kutoka kwa Kampuni ya Songoro Marine ya Jijini Mwanza iliyotengeneza Kivuko hicho na kukamilisha matengenezo mpema mwezi Juni mwaka 2018.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi Issack Kamwele (Kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Mhe, Antony Bahebe Masele wakati anawasili katika Kivuko cha Kigongo. (Kushoto) Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi,Fredrick Nyoka.
Akitoa taarifa ya Mradi huo Mtendaji Mkuu wa TEMESA,Dkt, Mussa Mugwatu alisema kuwa Kivuko hicho kimetengenezwa kwa shilingi Billioni 8.9 ambazo ni fedha za Tanzania na kina uwezo wa kubeba tani 250 ambayo ni abiria 1000,Magari 36 na kubainisha kwamba eneo hilo la Kigongo na Busisi lilikuwa limezidiwa na abiria katika utaoaji wa huduma na waliweka mikakati ya kutengeneza Kivuko kipya.
(Kulia ) Kivuko cha MV.MWANZA kinaonekana kimetua kwa ajili ya kupokelewa rasmi katika Kivuko cha Kigongo Wilayani Misungwi
Wazri Kamwele,aliwataka Wanachi wa Misungwi na Mkoa wa Mwanza kukitumia vizuri kivuko hicho katika kujipatia maendeleao ya dhati ya kiuchumi na kijamii na kueleza kuwa Serikali hadi sasa imefikisha vivuko 36 kwa Tanzania nzima.
Katika mapokezi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalmbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Wakuu wa Wilaya,YA Kwimba,Sengerema na baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala ,taasisi na Mashirika ya Umma,Wenyeviti wa Halmashauri, na Wakurugenzi wa Halmashauri zaMkoa wa Mwanza, Madiwani na Viongozi wengine wa Dini.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.