Serikali kujenga uzio ili kukabiliana na uvamizi wa makundi ya wafugaji katika shamba la mifugo Mabuki wilayani Misungwi mkoani mwanza.
Hayo yamebainishwa na Naibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Alexender Mnyeti leo wakati akizungumza katika kikao na Viongozi na Vijana wa BBT katika kituo atamizi cha Mabuki,mara baada ya kupewa taarifa ya uvamizi wa mara kwa mara wa makundi ya mifugo kutoka kwa wafugaji Kata za Misasi,Kijima,Mabuki na Kata za Wilaya za jirani.
Mhe.Myeti amesema Wizara itaweka utaratibu wa kujenga uzio kuzunguka shamba la mabuki lenye ukubwa wa eneo la hekta zaidi ya elfu tisa ambapo ujenzi huo utajengwa kwa awamu kuanzia maeneo ya Kata zenye uvamizi mkubwa ikiwemo Kata ya Kijima na Misasi ili kukabiliana na kukomesha uvamizi wa mifugo kwenye hifadhi ya shamba la Mabuki.
"Hii ni rasilimali ya nchi siyo ya Misungwi pekee na ni muhimu shamba likalindwa kwa manufaa ya wote" alisisitiza Mnyeti.
Mhe. Naibu wa waziri wa Mifugo na Uvuvi ameongeza kwamba Wizara itaweka bajeti ya kujenga ujizio kwa awamu ili kuepusha mwingiliano wa mifugo ya asili na mifugo ya Serikali pamoja na mradi wa ki mkakati wa Vijana wa BBT ili kuepusha mlipoko wa magonjwa ya mifungo yanayo tokana na mwingiliano wa makundi ya mifugo ya wananchi.
Mhe.Mnyeti ameeleza kwamba Serikali itatoa fedha za kujenga na kukarabati malambo ili kupata huduma ya maji na kuwata wataalamu waendelee kutoa elimu ya kutosha kwa wafugaji ili waweze kufuga kisasa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Alexender Mnyeti amefanya ziara ya kutembelea na kuongea na vijana wa BBT katika shamba la Mifugo Mabuki leo akisikiliza na kutoa maelekezo ya Serikali ambapo amesema Serikali itajenga uzio kuzunguka shamba la mifugo Mabuki Wilayani Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.