Serikali ya Canada chini ya Shirika la Agriteam Health Tanzania la Mradi wa Mama na Mtoto Wafadhili Gari la Wagonjwa (Ambulance) yenye thamani ya Milioni 143 kwa Halmashauri ya Misungwi ili kupunguza Vifo vya Wajawazito na Watoto chini ya umri wa miaka 5
Akikabidhiwa Gari hilo la Wagonjwa toka kwa Meneja Mradi wa Mama na Mtoto ulio chini ya Shirika la Agriteam Helath Tanzania Bi,Tanya Salawski, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hii Eliurd Mwaiteleke alisema kwamba ni faraja kubwa kwa Halmashauri kupata Ambulance ambayo itasaidia na kupunguza Vifo vya Wagonjwa wanaohitaji kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya na Rufaa wakiwemo akina Mama Wajawazito na Watoto wenye umri chini ya miaka mitano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri aliwashukuru kwa msaada huo na kuwataka kuendelea na ushirikiano katika kusaidia ufadhili wa Vifaa mbalimbali pamoja na kuendelea na utoaji wa Mafunzo kwa watoa huduma za Afya yanayoendeshwa kwenye Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Wilayani ili kuwajengea uwezo watoa huduma hizo kuwa na uwezo wa kuwaelimisha Wananchi kuhusu masuala ya tiba bora na kuachana na mambo ya kimila hivyo waweze kuhudhuria kliniki na Vituo vya Afya kupata ushauri na matibabu halisi.
Mwaiteleke alieleza kwamba Shirika hilo limeanza kazi Wilayani Misungwi tangu mwaka 2016 na wameshaanza kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya wa ngazi za Vijiji kwenye Vituo mabalimbali vya kutolea huduma za Afya ambapo katika Wilaya nzima kuna Vituo 48 vya kutolea huduma za Afya .
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt, Zabroni Masatu alibainisha baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika shughuli ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na tatizo la Usafiri kwa Wagonjwa wa Rufaa ambalo kwa sasa wameweka Mikakati ya kutatua kwa kushirikisha Wadau na Wahisani mbalimbali na Wilaya hadi sasa ina jumla ya Magari ya Wagonjwa matano (5) yatakayosaidia katika utoaji wa huduma za dharura kwa Wagonjwa wa Rufaa.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.