Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miaka mitatu ya utawala wake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 alielekeza fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya sekta ya elimu kupitia mradi wa Boost wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1,512,500,000/= ambazo zimetumika katika mradi huo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara za Viongozi za ukaguzi wa miradi hiyo Wananchi wa Vijiji vya Mwagiligili, Busegeja na Mbela wamefurahishwa na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Boost ambapo miradi hiyo ililetwa kwa lengo la kutoa elimu bora kwa Wanafunzi kupitia ujenzi wa Madarasa yaliyojengwa, ujenzi wa vyoo pamoja na madawati uliotekelezwa kwa Shule za Msingi tisa Wilayani humo na wamempongeza na kumshukuru Rais wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha nyingi katika miradi ya elimu kwa muda mfupi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Joseph Mafuru amesema kwamba kupitia Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imefanikiwa kupata fedha shilingi Bilioni 1.5 kujenga shule za msingi mpya 2 na kukarabati shule zingine 7 ambapo Viongozi na Watendaji wamehakikisha fedha hizo zimetekeleza shughuli za ujenzi kwa wakati na kwa kasi ambayo inaridhisha ili kurahisisha shughuli pamoja na kuongeza kiwango cha elimu Wilayani na taifa kwa ujumla na kupunguza adha na kero kwa watoto kutembea umbali mrefu na mrundikano madarasani.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Mhe, Abdi Makange akiwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya katika Shule ya msingi Mwagiligili pamoja na Shule ya msingi mpya ya Shilabela Wilayani Misungwi amesema Watumishi wamejitahidi kusimamia ujenzi kwa uaminifu mkubwa na kuhakikisha miradi hiyo ya Boost Wilayani Misungwi inakamilika na inazidi kwenda vyema kwa kujengwa kwa kiwango cha hali ya juu na hatimaye kukidhi na kujibu changamoto za watoto kutokwenda shule kwa uhaba wa majengo ya madarasa pamoja na madawati.
Mhe, Makange amewasihi na kuwataka Wananchi na Wakazi wa Kijiji cha Mwagiligili na Kata ya Busongo pamoja na Wakazi wa Shule ya msingi Shilabela kuyatunza na kuyalinda madarasa ,madawati pamoja na vyoo ili kuwanufaisha wao na kizazi kijacho na kuwakumbusha Wazazi kuwahimiza na kuwapeleka watoto shule ili wapate elimu na maadili mema.
Naye Afisa Vifaa na Takwimu wa Shule za Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Mratibu wa Mradi wa Boost Bw. Godfrey Majura akitoa takwimu za fedha za miradi ya Boost amesema fedha zilizotolewa na Serikali kuu kwa Bajeti ya fedha ya mwaka 2022/2023 kwa ajili ya kutekeleza mradi ni shilingi Bilioni 1,512,500,000/= ambazo zililetwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya Elimu msingi ambapo zimeweza kunufaisha na kujenga na kukarabati miundombinu na majengo katika shule za msingi 9 ambazo ni Shilabela, Mwabebea, Mwagiligili, Chata, Igwata, Busegeja, Iteja,Kagera, na Nyabuhele .
Bw Godfrey Majura ameongeza kwamba Serikali ilitoa fedha shilingi Milioni 540.3 kujenga shule ya msingi mpya ya Shilabela pamoja na shule ya msingi Ntende kwa sasa shule ya msingi mpya ya Mwabebea ambayo imejengwa kwa shilingi Milioni 540.3 na shule za msingi 7 zilizobaki zimefanyiwa ukarabati wa miundombinu ya majengo pamoja na nyongeza ya kujenga majengo ya Madarasa na vyoo hivyo zoezi la ujenzi limefanyika vizuri na kwa ubora unaoridhisha kupitia kamati za ujenzi, manunuzi na mapokezi.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Misungwi akiwamo Bw, Samson Selema amesema kuwa hapo awali watoto walikua wakipata adha kubwa wakiwa darasani kwani iliwabidi kujazana hatimaye hali hiyo kwa sasa imetatuliwa ambapo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Misungwi kwa wakati huo Mhe. Paulo Chacha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo katika sekta zote ikiwemo elimu, Afya na Maji na kuwaomba waendelee na moyo huo ili kuwaletea maendeleo ya dhati Wananchi.
Halmashauri ya Misungwi imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya, Barabara, Maji pamoja na sekta ya Elimu ambapo kwa upande wa elimu kupitia mradi wa Boost imeweza kutekeleza shule hizo pamoja na kuendelea na utekelezaji wa miradi mingine ya elimu Sekondari.
Mwonekano wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya msingi Shilabela iliyopo Kata ya Misungwi ambayo imegharimu zaidi ya kiasi fedha shilingi Milioni 500 fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa BOOST.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.