Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza yapokea msaada wa Vifaa vya kufundishia na kujifunzia kutoka kwa Kampuni ya Nebrix Ltd yenye Makao Makuu Jijini Mwanza kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Serikali Wilayani humu.
Akizungumza katika makabidhiano ya msaada wa vifaa hivyo ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Afisa Masoko wa Kampuni ya Nebrix Ltd, Mwanza, Ayubu Robert Ng”hwelo amesema kwamba msaada huo ni pamoja na Vitabu 50 mchanganyiko vya masomo mbalimbali, Global 1, Dustbin 5 za kuhifadhia taka laini, Heart Model 1, Charts 20, First Aid Kit 1, na Skeleton Model 1.
Afisa Masoko, Ayubu Robert, wa Kampuni ya Nebrix Ltd ya Mwanza ameeleza kwamba Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi 4,300,000/= ambapo vyote vitatumika kufundishia na kujifunzia kwa Walimu na Wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Misungwi zenye upungufu na uhaba wa Vifaa hivyo na vitasaidia kuboresha utendaji kazi na kuinua kiwango cha taaluma kwa Wanafunzi Wilayani humo.
Bw, Philipo Andrea(kulia) Afisa Masoko wa Kampuni ya Nebrix Ltd akimkabidhi na kutoa maelezo ya Vifaa vya kujifunzia na kufundishia Wanafunzi wa Sekondari, Bi, Dianah Kuboja Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Misungwi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba amesema kuwa katika Halmashauri ya Misungwi kuna Shule za Sekondari 30 ambapo Shule za Serikali ni 25 na Shule za Sekondari za binafsi ni 5, hivyo mahitaji ya Vifaa vya kujifunzia na kufundishia ni muhimu na vinahitajika sana, hivyo amewashukuru na kuwapongeza Kampuni ya Nebrix Ltd ya Mwanza, kwa maamuzi ya kutoa msaada huo katika Halmashauri ya Misungwi,.
Bw, Kisena Mabuba aliongeza kuwa Kampuni hiyo imefanya vizuri kwa kukumbuka kuwasaidia Wateja wake kwa kutoa Vifaa wezeshi kutokana na faida ya mapato yanayotokana na shughuli yao ya usambazaji wa Vifaa vya Maabara na Kemikali katika Shule za Sekondari, na kwamba Vifaa hivi vitawasaidia sana Wanafunzi kujifunzia na hivyo kuinua kiwango cha taaluma katika Shule za Sekondari hususan katika Shule zenye upungufu wa Vifaa husika.
Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bi. Dianah Kuboja amesema kwamba Vifaa hivyo vyote vitapelekwa katika Shule za Sekondari mpya ambazo ni J Magufuli Sekondari pamoja na Mamaye Sekondari, Shule hizo zina uhaba na upungufu mkubwa wa Vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa Wanafunzi na Walimu , hivyo vitawasaidia sana na hatimaye kuboresha taaluma katika Shule hizo.
Bi, Kuboja alieleza kwamba Vifaa hivyo vitaongeza pia kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Wilayani Misungwi ambapo kwa upande wa ufaulu wa Mitihani ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2018 , Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ilikuwa katika nafasi ya 4 Kimkoa kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza .
Kampuni ya Nebrix Ltd yenye Makao Makuu Jijini Mwanza imeanzishwa rasmi mwaka 2007 na inajuhusisha katika shughuli za usambazaji wa Vifaa vya Maabara, Kemikali pamoja na Vifaa vya kujifunzia na kufundishia na ina matawi mbalimbali katika Mikoa 10 kwenye maeneo ya Shinyanga, Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe, Songea, Kasulu, Ifakara, Mpanda, Sumbawanga , Dar Es Salaam na Mwanza.
Bi, Dianah Kuboja Afisa Elimu Sekondar Wilaya ya Misungwi akifurahia Msaada wa Vifaa baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Nebrix kupitia kwa Bw, Ayub Robert ambaye ni Afisa Masoko
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.