Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Mhandisi Robert Gabriel apongeza usimamizi na utekelezaji wa Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhandisi Robert Gabriel amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutembelea na kuona shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zilizofanyika kwa mwaka 2020/2021 katika Halmashauri hiyo yenye jumla ya Kata 27.
Mhandisi Robert Gabriel amesema kwamba usimamizi wa matumizi ya fedha za umma unaridhisha na katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatekekelezwa kikamilifu hususani katika miradi inayotolewa fedha na Serikali na nguvu za Wananchi akizungumza katika mradi wa ujenzi wa maabara 3 katika Shule ya Sekondari Sanjo ambapo Jengo la maabara lenye vyumba vitatu limekamilika kwa gharama ya shilingi .117,000,000/= kati ya fedha hizo shilingi 60,000,000/= ni kutoka Serikali kuu na shilingi 57,000.000/= ni nguvu na michango ya Wananchi wa Kata ya Usagara.
Ameweza kutembelea pia katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ambapo tayari ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi umekamilika na Jengo linatumika kwa kulaza Wagonjwa ambao ni akina Mama wajawazito, Jengo hilo limejengwa kwa msaada wa Wafadhili wa Impact wa Nchini Canada, pamoja na kuona mradi wa utafiti wa Malaria wa PAMVERRC ambao unafanya utafiti wa njia za kuzuia malaria katika Kata 17 za Wilaya ya Misungwi.
Mhandisi Gabriel amewataka Watendaji kuongeza ushirikiano kwa kufanya kazi kama timu na kwa kufanya hivyo kutaongeza na kuleta maendeleo makubwa zaidi na miradi itataekelezwa kwa umakini na ubora zaidi, amewataka kufanya kazi kwa moyo na kujituma kwa weledi hatimaye kufikia malengo na dira iliyokusudiwa.
Awali akizungumza na Wananchi katika maeneo tofauti ya Vijiji vya Nyanghomango na Usagara amewatahadharisha na kuwataka Wananchi na Viongozi Wilayani humo na Mkaoni Mwanza kwa ujumla kuchukua tahadhari kubwa na kukabiliana na mlipuko wa wimbi la tatu la Ugonjwa wa Covid 19 usababishwao na Virusi vya Corona ambao umeanza kuzikumbuka nchi za Afrika na kuwaomba kuendelea kuzingatia masharti na maelekezo ya Watalaam wa Afya ikiwa ni pamoja na kunawa Mikono, Kuvaa Barakoa, kuepuka Mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kukaa umbali wa zaidi ya mita moja na nusu baina ya mtu na kufanya mazoezi
Mhandisi Robert Gabriel ameongeza kwamba endapo Wananchi wataona dalili zitokanazo na Ugonjwa huu wa Corona ikiwemo kuumwa kichwa, kikohozi, Mafua makali, Mwili kuchoka, kutonusa harufu, na kubanwa mbavu wawahi mapema katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kwa matibabu na kuendelea kuwakinga wengine.
Katika ziara hiyo ya kutembelea shughuli za miradi Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameambatana na Wajumbe wa Kamati ay Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misungwi, Watendaji na Wataaalam.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyanghomango Wilayani Misungwi wakati wa ziara ya kikazi ya shughuli za maendeleo hivi karibuni
Jengo la Vyumba viwili na ofisi moja ya Walimu lilojengwa katika Shule ya Sekondari ya Nyangh"omango ambalo limekamilika tayari na litazinduliwa na Kiongozi wa Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.