Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhadisi Robert Gabriel afanya ukaguzi na kuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa 146 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Akikagua miradi hiyo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mawematu, Shule ya Sekondari Misungwi pamoja na shule ya Sekondari Sanjo Mhandisi Robert Gabriel ametoa maelekezo kwa Viongozi na Watendaji kuendelea kusimamia kikamilifu ujenzi huo kwa kuzingatia vipimo,mchoro na ramani ya majengo, kuzingatia uwiano wa mahesabu katika vipimo vya ujenzi wa majengo ya Serikali kulingana na taratibu na kanuni za kitaalam ili kuweza kukamilisha majengo ya madarasa kwa usahihi ubora pamoja na thamani ya fedha kuweza kuonekana.
Mhandisi Robert Gabriel amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kutembelea na kuona shughuli za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa fedha shilingi Bilioni 2.9 iliyotolewa na Serikali katika Halmashauri hiyo kutekeleza jumla ya madarasa 146 yanayojengwa katika shule 32 za Halmashauri hiyo.
Mhandisi Robert Gabriel amesisitiza Watendaji kusimamia vizuri ubora na kiwango cha ujenzi wa majengo ya madarasa na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuhakikisha miradi ya madarasa yote inatekekelezwa kikamilifu , akizungumza katika mradi wa ujenzi wa madarasa 6 katika Shule ya Sekondari Mawematatu ambapo ujenzi umefikia hatua ya boma na unaendelea katika hatua ya uwekaji wa jamvi na kuezeka ameshauri Halmashauri kuwatumia katika kujenga vijana wa Chuo cha Maendeleo ya jamii ufundi cha Misungwi na kuwapatia maeneo ya kujenga ili kuweza kusaidia na kuwapa uwezo na kuaminiwa na jamii na hatimaye kuunda vikundi vya ujenzi ambavyo vitafanya shughuli za Ujenzi wa majjengo ya Serikali na kuweza kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Mhandisi Robert Gabriel amewataka Watendaji kuongeza ushirikiano kwa kufanya kazi kama timu na kwa kufanya hivyo kutaongeza na kuleta maendeleo makubwa zaidi na miradi hiyo itataekelezwa kwa umakini na ubora zaidi, amewataka kufanya kazi kwa moyo na kujituma kwa weledi hatimaye kufikia malengo na dira iliyokusudiwa.
Katika ziara hiyo Mhandisi Robert Gabriel ameushukuru Uongozi wa Benki ya CRDB Taifa kwa kuonyesha upendo na kuweza kurudisha asante kwa Wananchi kwa kutoa madawati kwa kusaidia Wanafunzi kujisomea vizuri na kuwahakikishia kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuleta mendeleo kwa Wananchi pamoja na juhudi za taasisi za fedha katika kuinua uchumi wa taifa.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta amesema kwamba Benki imeweza kukabidhikwa Mkuu wa MKoa wa mwanza madawati 145 yenye tahmani ya Milioni 10 ambapo wameweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya Elimu na wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misungwi, pamoja na Watendaji na Wataaalam wa Halmashauri ya Misungwi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Katikati akizungumza na kuishukuru benki ya CRDB kwa kutoa madawati 145 kwa Hallmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja na meneja wa Benki ya CRDB Lusingi Sitta ( wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bi. Leokadia Humera pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Petro Sabatto amabye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronika Kessy katika Hafla hiyo
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.