Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla aagiza kukamilishwa Kwa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3 ili kuruhusu Huduma za upasuaji na huduma zote kuanza kutolewa.
Mhe, Makalla amewaagiza Viongozi na wasimamizi wa mradi huo kukamilisha kwa wakati ifikapo Disemba 31, 2023 ili huduma zinazosubiriwa zianze kutolewa Kwa Wagonjwa.
Mhe. Makalla amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo kwa kuwajali Wananchi wa Wilaya ya Misungwi kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya kwenye kijiji cha Iteja ambayo inaendelea vizuri na imefikia hatua za mwisho za Ukamilshaji..
"Mhe, Rais Samia hakika amefanya kazi kubwa sana Misungwi, nimeona na kuthibitisha ujenzi wa kiwango kikubwa sana wa majenga zaidi ya 14 kwenye hospitali hii pamoja na vifaa tiba kama mashine ya Mionzi sasa naomba sote kwa pamoja tushiriki katika kukamilisha ujenzi huu." Amesema Mhe. Makalla
Mhe. Makalla pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakati akigakua ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mwabebeya iliyojengwa katika Kijiji cha Nyang'homango Kata ya Usagara ikwa ufadhili wa mradi wa kuimarisha elimu ya Awali na Msingi 2022/23 (BOOST) kwa gharama ya shilingi Milioni 540 Hadi kukamilika.
Mhe, Mkuu wa Mkoa huyo ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imeweza kutekeleza Mradi huo kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi Kwa Kiwango na ubora na kukamilisha ujenzi kwa wakati.
" Hakika mmefanya kazi kubwa, tuliambiwa madarasa haya yakamilike kabla ya mwezi wa 12 lakini nyie mmekamilisha kabla ya wakati, hongereni sana, Amesema Mhe,Makalla
Aidha, amesema hakuna sababu ya mtoto kukaa mtaani hivyo Wananchi wawapeleke watoto shule waweze kujiunga na shule hiyo ambayo itaondoa adha ya msongamano kwenye shule zingine za Kata ya Usagara.
Mhe, Makalla amemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi BwJoseph Mafuru kuhakikisha mchakato wa kumpata Mwalimu Mkuu Mwenye sifa stahiki wa shule hiyo unafanyika Kwa haraka na kuwezesha Maendeleo ya Shule hiyo katika taaluma mwaka 2024.
Ameelekeza Tannesco Wilaya ya Misungwi kuhakikisha wanatoa Ushirikiano katika hatua za kuweka miundombinu ya umeme katika Shule hiyo ya Msingi Mwabebeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla katikai,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Paulo Chacha na wa kushoto ni Afisa Elimu Msingi Bw.Chrisopher Legonda akikagua Mradi wa Shule mpya ya Msingi Mwabebeya iliyopo Kijiji cha Ntende Kata ya Usagara iliyogharimu zaidi ya Milioni mia tano kwa Fedha za Serikali kupitia mradi wa BOOST.
Mwonekano wa majengo ya Shule ya Msingi ya Mwabebeya iliyopo kijiji cha Ntende kata Usagara ambayo imejengwa kwa Fedha za Serikali kupitia Mradi wa BOOST ambayo imeharimu zaidi ya Milioni mia tano.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.