Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel aagiza kukamatwa wadaiwa sugu wa makusanyo ya Mapato ya ndani shilingi Milioni 48 na kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ndani ya mwezi mmoja Wilayani Misungwi.
Mhe, Mkuu wa Mkoa Robert Gabriel ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022
Mhandisi Robert Gabriel amewatakaViongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha Watumishi hao wanaodaiwa fedha hizo wanarejesha mapema fedha za Serikali ambapo waangalie pia mikataba yao na kuona Wadhamini wao ili waweze kutoa fedha za makusanyo ya mapato ya ndani wanayodaiwa ili ziweze kutumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Misungwi.
Amesema kwamba fedha za mapato ya ndani shilingi 48,316,205/= zilizokusanywa kwa nyakati tofauti na Wakusanya mapato wa Halmashauri hiyo wakiwemo Watumishi na wakusanyaji wengine wa mapato walioingia mikataba ya kukusanya mapato husika.
“ Lazima msome tabia za Makala wanaokusanya fedha za mapato na kujiridhisha na uhalali na nyendo zao na kuhakikisha wanajiridhisha fedha za mapato kwa wakati”. Alisisitiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza..
Ameeleza kuwa vyombo vya uchunguzi wawasake wote na warejeshe fedha zote za makusanyo ya mapato ya ndani na kuwataka Watumishi wote wanaodaiwa fedha za mapato wakatwe kutoka katika mishahara yao pia wajiridhirishe katika kudhibiti fedha za mapato yasivuje na kuimarisha mifumo na kuweka mikataba makini na kuagiza suala hilo lishughulikiwe kwa wakati ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande wake Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi limeridhiria agizo hilo la Mkuu wa Mkoa la kuwakamata wadaiwa sugu wa makusanyo ya fedha za mapato pamoja Wadaiwa wa madeni ya mikopo ya Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ambazo ni fedha za Vikundi shilingi milioni 83.9 ambazo walikopeswa kwa muda lakini hawajweza kurejesha fedha hizo kwa wakati.
Baadhi ya Madiwani akiwemo Diwani wa Kata ya Sumbugu Jogoli Mayombo alieleza kwamba wadhamini wa kukusanya mapato wanaodaiwa wakamatwe kwa mujibu wa mkataba pamoja madeni ya vikundi vya mikopo mbalimbali virejeshe ili fedha hizo vipewe na Vikundi vingine.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakinyosha mikono ishara ya kuridhia maelekezo na maagizo ya Mhe, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Mkutano wa Braza la Hoja za Mdhbiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2020/2021 za Halmashauri ya Wilaya hiyo. Aliyeketi katikati ni Mhe, Joel Dogani Diwani wa Kata ya Mbarika .
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Robert Gabriel amesema kwamba fedha hizo hazikuwa zawadi hivyo walipe ili ziweze kukopeshwa kwa Vikundi vinavyohitaji Mkopo huo wa Serikali ambao hauna riba na kwamba Halmashauri ya Misungwi iweke mipango mikakati ya udhibiti wa matumizi ya fedha za miradi na kuhakikisha inatekeleza kikamilifu miradi na kuwapatia maendeleo Wananchi.
Awali akiwasilisha taarifa ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo amesema kwamba katika ukaguzi huo Halmashauri hiyo imepata Hati ya kuridhisha (Hati safi) ambapo hoja zilizohojiwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zinaendelea kutekelezwa.
Bw, Mihayo ameeleza kwamba kulikuwa na Hoja za nyuma ambazo ni 35 ambapo Hoja 10 zimefungwa na Hoja 23 zinaendelea kutekelezwa na Hoja 2 ambazo hazijatekelezwa na Menejimenti inaendelea kufuatilia hoja hizo na kuzitekeleza na baaadae kuhakikiwa na Wakaguzi na watahakikisha zinafanyiwa kazi na kukamilisha kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.
M
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe, Rahma Fidel akizungumza kwa msisitizo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani mapema leo na kushoto ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi Chollage A Chollage na kulia ni Mkuuw amKoa wa Mwanza Mhndisi Robert Gabriel ambaye amezungumza na Braza la Madiwani wa Halamshauri ya Misungwi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi, Bw, Benso Mihayo (aliyesimama Kulia ) akieleza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri mapema leo
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.