Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Adam Malima aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mwawile kwa kutumia fedha zaidi ya shilingi milioni 400 za mapato ya ndani Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Rais,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuboresha afya za Wananchi imeendelea kuleta neema katika sekta ya afya kwa kutoa fedha za kujenga Vituo vya afya na Zahanati ambapo kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa mwaka wa fedha wa 2022 na mwaka 2023 imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 500 za ujenzi wa jengo la OPD, Jengo la Maabara, na jengo la Wodi ya Wazazi ambayo yote kwa sasa yamekamilika kwa asilimia 85 na hatua za ukamilishaji zinaendelea vizuri.
Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Nhundulu Wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Adam Malima amesema kwamba Wananchi wa Wilaya ya Misungwi wamekusanya fedha kutokana na ushuru wa mazao na mapato mengine na kuamua kujenga Kituo cha Afya kwa ajili ya utoaji wa huduma za Afya Wananchi.
“Wananchi wa Kata ya Nhundulu mmepata kinachowastahili kutokana na jitihada zenu, fedha hizo zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotumika kujenga majengo hayo si kidogo zimetokana na ushuru wa mazao yenu ambazo zimechangia kutokana na mapato ya Halmashauri, hongereni kwa jitihada hizo.’¯Alieleza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe, Malima aliagiza Shirika la Umeme TANESCO kuwafungia umeme katika Kituo hicho ili kianze kutoa huduma vizuri kwa kupata huduma ya umeme na kuweza kusaidia katika huduma za upasuaji.
Imeelezwa kwamba Wananchi zaidi ya 10,000 (elfu kumi) wa maeneo ya Kata ya Nhundulu na vijiji jirani vya Halmashauri ya Shinyanga vijijini wanatarajiwa kunufaika na huduma za Afya mara baada ya Kituo cha Afya cha Mwawile kuanza kutoa huduma.
Alisema ujenzi wa miradi ya vituo vya afya inayohusisha miundombinu ya wodi za wazazi,watoto,maabara na majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) haviwezi kutoa huduma bila kuwa na maji ya kutosha hivyo ni muhimu Halmashauri ya Misungwi na Wakala wa Maji vijijini RUWASA washirikiane kutafuta fedha za kuchimba visima virefu vya maji katika Kituo hicho kabla ya kuanza kutoa huduma.
Pia alimwaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha Kituo hicho kinafunguliwa na anapeleka Watumishi wa kutosha, vifaa tiba, na madawa kwenye kituo hicho ili wananchi wapate huduma ya Afya kwa wakati
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana alieleza kuwa amefurahishwa sana na hatua za ujenzi wa Kituo hicho na kwamba atahakikisha anafuatilia kwa karibu hatua zote za ukamilishaji na kufunguliwa kwa huduma za Afya katika Kituo hicho ikwemo na upatikanaji wa Watumishi na vifaa tiba kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Adam Malima ( wa pili kulia) akipokea maelezo namna ya miradi kutoka kwa Mhandisi Godfrey Sanga Meneja wa RUWASA Mkoa (wa pili kushoto)pamoja Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana ( wa kwanza kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Matiko Chacha (wa kwanza kulia) wakati akikagua miradi mbalimbali Wilayani Misungwi
Baadhi ya majengo ya Kituo cha Afya Mwawile ambacho kimejengwa kwa Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kiasi cha shilingi Milioni 400.ambayo nimwonekano wa Majengo ya Mabara na Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) kwa sasa ujenzi upo asilimia 89 na wanaendelea na ukamilishaji.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.