Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe, Amos Makalla aagiza Halmashauri ya Misungwi kuzitumia kikamilifu fursa za miundombinu ya uwekezaji unaofanyika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Amos Makalla katika ziara ya kujitambulisha na kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi Wilayani Misungwi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha yanasimamiwa vizuri na kuelekezwa kwenye Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema hayo katika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi ambapo ametoa dira ya maendeleo katika kuwahudumia Wananchi kufuatia kuteuliwa hivi karibuni na Mhe,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kuongoza Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza na Watumishi Wilayani Misungwi ametoa rai kwa Viongozi na Watumishi wote kuwa na nidhamu na kujituma kwa bidii katika utendaji kazi na kwa kupokea na kutatua changamoto kwa wakati kwa wananchi ili waweze kupata huduma bora.“Sifa ya Kiongozi ni kutoa matumaini ya watu anaowaongoza “
Aidha Mhe,Makalla amewataka watendaji wote kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia kikamilifu Miradi yote ya Maendeleo na kuwashirikisha Wananchi mafanikio ya miradi hiyo ikiwa pamoja na kuboresha Sekta ya Elimu ya Msingi na Sekondari na kuhimiza watoto kwenda shule kupata elimu bila malipo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paul Matiko Chacha amesema kuwa kwa ushirikiano wa Watumishi waHalmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja Timu Menejimenti kwa ujumla wake Halmashauri inaendelea kukusanya Mapato ya ndani kwa bidii zote na kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Bw.Chacha ameongeza kwamba kupitia Miradi mbalimbali ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ambayo ni Reli ya kisasa SGR na Daraja la Kigongo Busisi itaimarisha uchumi wa Wilaya ya Misungwi pamoja na Mikoa jirani.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya kwa niaba ya Madiwani amempongeza kwa kuteuliwa kwake na kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Amos Makalla kwa ujio wake na kumhakikishia kwamba watahakikisha wanasimamia kikamilifu Mapato ya ndani ya Halmashauri ili kufikia malengo waliojiwekea kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paul Matiko Chacha kushoto akimkabidhi ya Taarifa ya Miradi ya Maendeleo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Amos Makalla wakati wa ziara yake ya kujitambulisha katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musungwi tarehe 3 Juni siku ya Jumamos.
Baadhi wa Wakuu wa Idara na Vitengo na Watumishi mbalimbali waliohudhuria katika Hafla fupi ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Amos Makalla wakisikiliza na kupokea maelekezo hayo katika Ukumbi wa Halmashauri siku ya Jumamosi tarehe 3 Juni 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Amos Makala akisalimiana na baadhi ya viongozi ngazi ya Wilaya wakati wa Ziara ya yake ya kujitambulisha kwa Watumishi na kutoa dira na Mwelekeo wake kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.