Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Amos Makalla aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa kupata Hati safi( Unqualified Opinion) katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Elikana Balandya katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mwishoni mwa wiki amesema kwamba Viongozi na Timu ya Menejimenti ya Halamshauri wameonyesha ushirikiano mzuri na kuendelea kupata Hati safi kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 na kuwataka kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi na ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Bw. Balandya amesema kuwa ni lazima Halmashauri isimamie vizuri ukusanyaji Mapato ya ndani ili kuzuia upotevu wa mapato na kufanya kaguzi za mara kwa mara ,usimamizi wa mzuri miradi mbalimbali ya maendeleo itasaidia ili kuondoa hoja za CAG.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,kashinje Machibya amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya misungwi imepata Hati safi kwa ushirikiano wa timu ya Waatam ,Wahe,Madiwani pamoja na watumishi wote kwa ujumla katika Halmashauri kwa kushiriana kwa juhudi na kufanya kazi kwa weledi na mshikamano na kutanguliza uzalendo mbele hivyo kwa umoja huo imepelekea Halmashauri kupata hati safi.
Aidha Bw,Machibya amewashukuru Waatam wote ngazi ya Halmashauri pamoja na Wahe,Madiwani kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa umoja kuwatumikia wananchi kwa nguvu zote na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya Sita na kwa maslahi ya mapana Taifa kwa ujumla.
Awali akiwasilisha taarifa ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 Mweka Hazina wa Halmashauri Bw. Joseph Mazito kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, amesema kwamba katika ukaguzi huo Halmashauri hiyo imepata Hati safi ambapo hoja zilizohojiwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zinaendelea kutekelezwa.
Bw,Mazito ameeleza kwamba kulikuwa na Hoja za nyuma ambazo ni 6 ambapo Hoja 1 imefungwa na Hoja 5 zinaendelea kutekelezwa ambapo Menejimenti inaendelea kufuatilia hoja hizo na kuzitekeleza na baaadae kuhakikiwa na Wakaguzi na watahakikisha zinafanyiwa kazi na kukamilisha kwa kipindi kifupi.
Mweka Hazina wa Halmasahuri ya Wilaya ya Misungwi Bw,Joseph Mazito akisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ya Wilaya ya Misungwi wakati wa kikao cha Hoja za CAG katika Ukumbi wa Halmashauri hivi karibuni.
Wahe,Madiwani wasikiliza kwa makini mjadala na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 katika ukumbi wa Halmashauri mapema wiki hii,ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ilipata hati safi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.