Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe, Paulo Matiko Chacha aawaga Watumishi na kuwashukuru kwa unyenyekevu mkubwa,ushrikiano walioonyesha katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Hayo ameseyasema Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe,Paulo Chacha jana tarehe 08, Aprili,2024 katika hafla ya makabidhiano katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ambapo amewashukuru watumishi wote kwa ushirikiano ambao waliutoa kwake wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano huo kwa Mkuu wa Wilaya mpya katika kutekeleza majukumu ya serikali na kuwahudumia wananchi.
Mhe,Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameongeza kwa kusema kuwa kuheshiamiana na kujituma katika kazi ndiyo nguzo ya mafanikio,na kuwataka watumishi kuwajibika kila mtu kwa nafasi yake ili kuondokana na migogoro siyokuwa na tija katika kutekeleza majukumu ya kila siku.
Aidha Katika Hafla hiyo Mhe. Paulo Chacha amewashukuru Viongozi na Watendaji kwa ushirikiano waliouonyesha kipindi cha Uongozi wake,kuwaomba waendelee na Moyo huo na kumpa Ushurikiano Mkuu Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi katika kuendeleza gurudumu la Maendeleo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Johari Samizi amesema kuwa ataendeleza yale yote yaliyo mazuri na kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na kuwatakaWatumishi wampe ushirikiano katika utendaji kazi wake na kumtakia kila kheri Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ametoa pongezi za dhati kwa Mhe,Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa Kuendelea Kuamini na Kumteua Ndg Paulo Chacha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na kuahidi kumpa ushirikano katika kuteleza majukumu ya kuwatumikia Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe,Paulo Chacha akiongea na watumishi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi jana ambapo aliwataka Watumishi kuendelea kuwa na ushirikiano katika utendaji kazi ili kuwatumikia wananchi.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza na kushiriki katika hafla fupi ya makabidhiano ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Paulo Chacha na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi katika Ukumbi wa Halmashauri jana ambapo Mkuu wa Wilaya alimpongeza na kumtakia kila kheri Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika kutekeleza Majukumu yake mapya ya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Paulo Chacha katikati,Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe.Kashinje Machibya na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tabaora jana katika Ofisi za Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.