Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makalla awataka Wanawake kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika miradi ya Maendeleo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mheshimiwa Makalla ameyabainisha hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya kilele cha siku ya Wanawake duniani iliyofanyika kimkoa wilayani Misungwi katika viwanja vya amani ambapo ametoa wito kwa wanawake wote kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza miradi mbali mbali ambayo inatekelezwa na Serikali ili kuleta tija na kuharakisha maendeleo kwa Wananchi.
Makala amewataka wanawake kutumia vizuri mikopo wanayo kopeshwa na Serikali iwe yenye kuleta tija na kukuza kipato na kuongeza ajira kwa watu wengine na kabla kupatiwa fedha hizo wapewe elimu ya namna ya kutumia fedha hizo.
“Haiwezekani unachukua hela ukafanye biashara wewe unaenda kununua makochi,makochi yatakusaidia kuleta hela?” alisisitiza Mhe.Amos Makalla.
Aidha Mkuu wa Mkoa Makalla amesisitiza kuongeza jitihada za utoaji wa elimu kuhusu faida ya kupima afya zetu na njia za uzazi wa mpango na afya uzazi,hedhi salama pia kujinga na maambukizi ya UKIMWI.
Sambamba na hayo amewakumbusha Wanaume kuendelea kuona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika masula ya uzazi na mapambano ya UKIMWI ambapo hali ya maambukizi kwa Mkoa wa Mwanza yamefikia aslimia 7.2 ikiwa waathirika wakubwa ni Wanawake na wasichana; na Serikali imetoa mwongozo kwa uanzishwaji na uendeshaji wa dawati la jinsia ili kutokomeza vitendo vya kikatili vya kijinsia katika maeneo ya umma.
Maadhimisho hayo yaliambatana na kaulimbiu ya Wekeza kwa wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na usatawi wa jamii.
M
Baadhi ya Wanawake kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mwanza, Taasisi na Mashirika ya Umma walioshiriki Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika tarehe 8/03/20240 katika viwanja vya Amani Wilayani Misungwi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.