Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka Wataalam wa Afya kuhakikisha wanapunguza na kutokomeza Vifo vya Mama na mtoto kwa kuboresha na kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma za Afya vituoni Mkoani Mwanza.
Bw, Elikana amewataka kuhakikisha Wataalam hao wa Afya wanalinda afya ya mama na mtoto muda wote, ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa mfumo wa kumfuatilia mama mjamzito mpaka hatua ya maandalizi ya kujifungua. uwepo wa vifaa vya kujifungulia vituoni, kujitahidi kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa Ujauzito, wakati wa kujifungua na watoto wachanga na ikiwezekana vifo hivyo vitokemezwe kabisa.
Wito huo umebainishwa wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa kwa Wataalam wa Afya wa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika tarehe 30 hadi 31 Januari 2023 katika ukumbi wa MGS Wilayani Misungwi, ambapo amesema idadi ya Vifo bado ni changamoto mwaka 2022 vifo vimeongezeka hadi kufikia 165,mwaka 2021 vifo vya akina mama vilikuwa 164 na vifo kwa watoto ni 1,948 kwa mwaka 2022 na 2021 vifo vya watoto vilikuwa 1,533 na kusissitiza juhudi zifanyike ili kutokomeza.
"Simamieni vifaa vya kujifungulia na kuhakikisha vinakuwepo vituoni muda wote, na Serikali imeendelea kutoa fedha za dawa na vifaa tiba kupitia MSD," Alibainisha Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza..
Amesisitiza kuwa asingependa kusikia mama au mtoto amekosa huduma kwa kisingizio cha kukosa dawa, na kutoa angalizo kuwa, mojawapo ya vipaumbele vya Serikali kupitia Sekta ya Afya kwa mwaka 2023 ni ubora wa huduma. za Afya na dhamiara kubwa ni kutokemeza Vifo vya akina Mama wakati ujazito ,kujifungua, na kuhakikisha Vifo vya watoto wachanga katika siku 28 za mwanzo na chini ya umri wa miaka mitano.
Pia Bw. Elikana amewakumbusha Wataalam hao kuhusu Majengo yaliyoelekezwa na Serikali kujengwa yakamilishwe na yaanze kutumika mara moja, Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ili vituo hivyo vikamilike kwa wakati,visajiliwe na vianze kutoa huduma ya afya kwa wananchi ambapo Serikali imewekeza fedha nyingi.
Bw, Elikana mewataka Wataalam wa AFya kuendelea na kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma kuhusu Bima ya Afya kwa wote na kusimamia utekelezaji ili elimu ya Bima ya Afya itolewe kwa wananchi kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na katika mikusanyiko na maeneo yote ambapo amewapongeza Sekta ya Afya Mkoani humo kwa utaratibu wa kufanya vikao kama hivyo vya kujadili maendeleo ya Sekta ya afya pamoja na changamoto zinazozikabili jamii na sekta ya afaya kwa ujumla.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa alieleza kwamba wamepokea maelekezo ya Katibu Tawala na kuanza kuyafanyia kazi na kuhakikisha kila Halmashauri inatekeleza yote yaliyoazimiwa na wamejipanga vizuri na imara katika kuhakikisha Sekta ya Afya inazidi kuwa na matokeo chanya kwa kuzingatia uwepo wa vifaa tiba na huduma bora. Katika vituo vyote vya Afya.
Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni kikao cha Robo Mwaka cha Wataalam wa Sekta ya Afya wa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza yaliyolenga kujadili Vifo vya mama vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhe, Elikana Balandya akizungumza na Wataalam wa Afya Katika kikao cha mafunzo ya kujengeana uwezo yaliyofanyika katika Wilaya ya Misungwi.
Baadhi ya Wataaalam wa Afya wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Viongozi kuhusu changamoto za sekta ya Afya
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.