Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe, Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa Maji wa Nyahiti – Misungwi wenye gharama ya shilingi Bilioni 13.77 unaohudumia Wananchi elfu 24,000 wa Kata ya Misungwi na Igokelo.
Mhe, Rais Samia akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Misungwi na amewapongeza kwa kupata maji safi na salama kwa asilimia 83 na kuelekea asilimia 100 kwa sasa na kuwaomba kuendelea kutunza mazingira na vyanzo vya maji na kuvuna maji ya mvua ili kupunguza tatizo la maji na baadae kuondoa kabisa tatizo la maji nchini.
Mhe, Rais Samia ametoa wito kwa Wananchi wote kuilinda na kuitunza miundombinu ya maji kutokana na kutumia fedha nyingi na Ameagiza Wizara ya Maji na Wahandisi wa mamlaka na Wakala za maji nchini kuhakikisha na kuongeza usambazaji wa maji kwa Wananchi ili waweze kupata maji na kunufaika na matunda ya raslimali za taifa na kuonya masuala ya kuwabambikia bili za maji wateja na kuhakikisha na kuwasisitiza Wananchi kuendelea kulipa bili kwa wakati kulingana na matumizi yake.
Akitoa taarifa ya Mradi huo wa maji Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji , Antony Sanga amesema kwamba Mradi huo wa maji umejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 13.77 ambao utanufaisha Wananchi elfu 24 wa Kata ya Misungwi na Igokelo .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Antony Sanga ameeleza kuwa mradi huo umejengwa kutoka katika chanzo cha Ziwa Victoria katika eneo la Kijiji cha Nyahiti ambao una uwezo wa kuzalisha maji zaidi ya lita za ujazo milioni nne na nusu.
Wakati huo huo, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemhakikishia Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ataendelea kufanya kazi kubwa ya kutatua na kukamilisha miradi ya maji ambayo imekwama na kukemea tabia ya Wataalam wa maji wanaowabambikia bili na kutoa gharama kubwa za kuunganisha maji kwa wateja.
Mhe, Aweso amewahakikishia Wananchi wa Mwanza na Usagara Misungwi kupata maji kutoka chanzo cha maji cha mradi wa Butimba ambao utasambaza maji katika maeneo ya Buswelu, Buhongwa pamoja na Usagara hadi Fella Wilayani Misungwi na Wizara imeelekeza Wakala na mamalaka za maji kutoa mipango na taarifa za maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maij katika Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri ili kuweza kuweka mikakati na mipango pamoja na usimamizi bora wa miradi husika.
Mhe, Rais Samia awali ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la JPM la Kigongo – Busisi linalojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 699 mradi ambao hadi sasa umefikia asilimia 27 za ujenzi pamoja na kuweka Jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa Reli ya kisasa (SGR) eneo la Fella kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka kwa gharama ya zaidi ya shilingi trioni 3.1 hadi kukamilika..
Msanii wa Nyimbo za Bongo Peter Msechu akitoa buraudani kwa kuimba wimbo maalum kuhusu maji katika Hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa mjini Misungwi uliofanyika katika tanki la maji la Masawe Mjini Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.