Serikali kupeleka Vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kuwezesha Wananchi kupata huduma bora za Afya Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan katika ziara yake akizungumza na wananchi katika eneo la Kigongo amesema kuwa Serikali itanunua Vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kama inavyofanya katika wilaya na maeneo mengine nchini kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Hayo yamejiri jana Juni,14,2023 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua mradi mkubwa wa Ujenzi wa daraja la JPM la Kigongo –Busisi lenye urefu wa Kilomita 3 na barabara ungamishi kilomita 1.66 ambapo wakati akijibu ombi la Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe,Alexender Mnyeti.
“Vifaa ya Wilaya vifaa vinakuja kila kinachopaswa kuwepo kitakuwepo pale,ninawashukuru wakandarasi kwa kazi kubwa wanayoifanya.”amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia amesema ujenzi wa daraja la JPM linalogharimu shilingi Bilioni 716 limefikia hatua za mwisho kwani mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 75 huku akiwaomba wananchi wa Misungwi kuendelea kutoa ushirikano wa kutosha kwa Mkandarasi wa ujenzi na amewaonya watu wanaodokoa vifaa na mali za ujenzi wa daraja hilo.
“Daraja hili limetoa ajira kwenu na litaendelea kutoa ajira maisha yote sababu ni kituo kikubwa cha magari yanayopita kwenda nje lakini yataenda pande mbalimbali za Tanzania.”amesisitiza Rais Samia.
Akizungumzia utekelezaji wa ujenzi wa daraja la JP Magufuli Rais Samia amewastaka vijana na watalaam wa kitanzania waliopata fursa za ajira katika mradi huo kujifunza na kupata ujuzi kutoka kwa watalaam wa kigeni ili baadaye waweze kusaidia Taifa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya aina hiyo wakati ujao.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe, Alexender Mnyeti wakati akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa Misungwi ameiomba Serikali kupeleka vifaa tiba vya kutosha katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kusaidia wananchi kupata huduma bora za afya ambapo tayri ujenzi wa Hospitali hiyo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.5 na ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za miradi ya Maji zaidi ya Bilioni 77 na utekelezaji unaendelea.
“Rais Samia Serikali imetupatia Wilaya ya Misungwi zaidi ya shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya miradi ya afya ,ujenzi wa Hospitali ya Wilaya imekamilika ,sasa tunaomba shilingi milioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ili wananchi waanze kufnuaika na utekelezaji wa mradi huu “alisisitiza Mhe. Mnyeti.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) nchini Mhandisi Mohamed Besta amesema ujenzi wa daraja la JPM lenye urefu km 3 litakapokamilika litarahisisha usafiri kwa majira ya mwaka kwa masaa 24 na kumaliza msongamano wa magari ulikuwa unatokea kwa kutumia vivuko na kupunguza muda wa kusafiri na kuchochea wa uchumi katika ukanda wa ziwa Victoria na Taifa kwa ujumla kwani mazao ya wakulima na mazao ya samaki yataenda sokoni kwa wakati.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya Mradi wa ujenzi wa daraja la JPM Juni,14,2023 kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa mradi wa daraja la JPM Abdulkarimu Majuto wakati akikagua daraja hilo litakalogharimu shilingi Bilioni 716 mpaka kuisha ambapo litasaidia kurahisisha usafiri pamoja na kukuza sekta ya uchumi hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la JPM hapo jana eneo la kigongo ambapo ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kufika tamati Februari,2024.
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakishuhudia na kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Mradi mkubwa wa daraja JPM eneo la Kigongo hapo jana ambapo ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 75.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.