Mradi wa Jengo la ofisi ya Uthibiti Ubora wa Shule wenye gharama ya shilingi millioni 134.5 umefunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe, Prof. Joyce Ndalichako (MB) katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ndalichako mapema leo amefungua Jengo la ofisi za uthibiti ubora wa Shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambalo limejengwa kwa muda wa miezi sita (6) kuanzia mwezi Mei 2019 na kukamilika mwezi oktoba 2019 baada ya Serikali kutoa fedha shilingi milioni 152 za ujenzi huo mapema mwezi Aprili mwaka huu 2019.
Jengo la ofisi ya Uthibiti ubora wa shule lilofunguliwa na Waziri wa Elimu ambalo limegharimu shilingi Milioni 134.5, tayari Watumishi wa Uthibiti ubora Wilaya ya Misungwi wameanza kunufaika na Mradi huu.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi, Mhe, Prof. Joyce Ndalichako amewataka Viongozi na Watendaji ngazi ya Mikoa, Wilaya nchini kuhakikisha wanafuatilia na kukaa na Wataalam, na Wadau wa sekta ya Elimu kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika suala la watoto wa shule Wavulana kwa Wasichana wanaoacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba zisizotarajiwa, kitendo ambacho kinasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini.
Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kwamba kwa mujibu wa taarifa za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi takwimu zinaonyesha kuwa na jumla ya Wanafunzi 3,838 ambao wameacha shule hadi kufikia mwezi Julai mwaka 2019 kutokana na sababu mbalimbaliza utoro na wengine kupata mimba za utotoni miongoni mwao watoto 2030 ni Wavulana na 1,808 ni Wasichana.
Akieleza na kufafanua zaidi kuhusu suala la elimu “ tatizo la kuacha shule limekuwa sugu hususani kwa watoto wa kike kutokana na tatizo la mimba lakini nashangaa sana mbona watoto wa kiume kuacha shule ndio wamekuwa wengi, tatizo ni nini, alihoji.” Waziri Ndalichako.
Amewaagiza Viongozi wa Mikoa na Wilaya kusimamia kikamilifu na kuweka mikakati madhubuti ya kutatatua changamoto na tatizo la watoto kuacha shule bila sababu ya msingi wakati Serikali inaendelea kutoa fedha za elimu bila malipo ambapo hadi sasa imeshatumia takribani kwa ajili ya kugharamia shughuli za elimu bila malipo hapa nchini pamoja na miradi ya ukarabati wa majengo na miundombinu uliofanywa na tayari umekamilika katika shule kongwe 68 za Sekondari ambapo Serikali inatarajia kufanya ukarabati katika shule za Sekondari 88 nchi nzima.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na Viongozi,Watendaji pamoja na Wananchi katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Uthibiti ubora wa shule Wilayani Misungwi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano imeweza kujenga majengo 100 ya ofisi za Uthibiti ubora wa shule hapa nchini kwa kutumia fedha shilingi Bilioni 15.2 na ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya kwa Watanzania.
Amewapongeza Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa kazi nzuri ya kusimamia vyema ujenzi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano na kuhakikisha jengo linakamilika kwa wakati kwa ubora na kiwango cha ujenzi na hatimaye wameweza kuwa na ziada ya shilingi million 17 ambayo itatumika katika shughuli zingine za maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.